Maajabu tisa ya msitu wa Amazon

Muktasari:

Katika maisha tunayoishi asilimia kubwa tunategemea misitu katika kuyaendesha, kungekuwa hakuna misitu ambayo hutuletea miti watu wasingetibiwa na wangekuwa wanapoteza maisha kwa sababu asilimia kubwa ya maisha haya tunayoishi tunapata dawa mbalimbali za kutibu magonjwa  kupitia misitu hiyo.


Katika maisha tunayoishi asilimia kubwa tunategemea misitu katika kuyaendesha, kungekuwa hakuna misitu ambayo hutuletea miti watu wasingetibiwa na wangekuwa wanapoteza maisha kwa sababu asilimia kubwa ya maisha haya tunayoishi tunapata dawa mbalimbali za kutibu magonjwa  kupitia misitu hiyo.

Kuna aina mbili za misitu, misitu ya asili ambayo miti yake hujiotea yenyewe bila kupandwa na binadamu na pia kuna misitu isiyo ya asili ambayo hupandwa na binadamu.

Msitu wa Amazon ni msitu wa asili ambao vitu vyote vilivyomo ndani ya msitu huo siyo vya kutengenezwa bali ni vya asili, ni msitu mkubwa duniani kote, ni msitu wa asili ambao ndani yake kuna maajabu mengi, ni msitu unaopatika katika Bara la Amerika ya Kusini msitu unaojumuisha mataifa tisa yaliyopo katika bara hilo ikiwa ni pamoja na Brazil, Peru, Colombia, Venezuela, Ecuador, Guyana, Suriname pamoja na Guyana ya Kifaransa.

Ni msitu ambao binadamu wanaishi na zaidi ya makabila 64 yapo katika msitu huo lakini cha kushangaza makabila 50 kati ya hayo hayajui chochote katika maisha haya tunayoishi mimi na wewe hapa. Wao wana maisha yao tofauti kabisa na sisi lakini ndani ya msitu huo kuna maajabu mengi ambayo wewe msomaji wa Mwananchi huenda haufahamu. Sasa ngoja nikujuze…

Anacconda

Wengi wenu mmemsikia au kumuona nyoka anayefahamika ndiye mkubwa duniani kote aitwaye Anacconda, ni nyoka anayesadikika kuwa na mpaka kilo 180 anapokuwa mkubwa na mwenye urefu wa futi za kufikia mpaka 30. Ni nyoka mkubwa lakini hana sumu kali. Nyoka hawa wapo wa aina nyingi  lakini  anayefahamika sana ni Anacconda wa kijani, unaweza ukakutana na nyoka huyo ukaogopa na kuanza kukimbia lakini ni nyoka ambaye mwendo wake ni  mdogo na kama wewe ni wa kujisahau unatakiwa uwe makini sana kwa sababu Anacconda hutembea pole pole sana kiasi cha kuweza kukuvamia bila wewe kufahamu.

Ukikutana na nyoka huyo ghafla na uko karibu na mto au maji usikimbilia huko kwa kuwa kasi ya Anacconda kwenye maji kubwa sana kuliko akiwa nchi kavu.

Watu wengi humwogopa Anacconda kwa kudhani kwamba anaweza kumtafuna lakini nyoka huyo ni nyoka anaependa kumeza nguruwe pori zaidi na mara chache sana ikitokea ndo humeza binadamu.

Nyoka huyu akishapata mlo wake anauwezo wa kukaa ndani ya mwezi mmoja bila kula chochote.

Mmea unaotembea

Mbali na Anacconda kupatikana kwenye msitu huo pia kuna mti unaofahamika kama mmea unaotembea ni mmea wa ajabu unaopatikana katika msitu wa Amazon na wengine hufikiria kwamba hutembea kama binadamu la hasha.

Mmea huo hutembea pole pole sana na huchipua kwa kufuata mizizi ya chini na baada ya miaka kadhaaa ukija kurudi sehemu ile uliyoona mmea huo unaweza kuona umehamia sehemu nyingine.

Electric Fish (Samaki wa umeme)

Samaki wanaopatikana katika msitu huo aina ya Electric Fish ni wenye shoti ya umeme ukiwashika vibaya unaweza rushwa kama umepigwa shoti, pia ni samaki wenye kilo hadi 21. Wana maajabu ya kuwa na umeme kwenye miili yao umeme. Siyo samaki wakorofi kwa kuwa hawapendi kula binadamu ila huwatesa sana mamba katika msitu huo ambao hujaribu kuwala.

Glass Frog (Chura wa kioo)

Vyura ni viumbe vinavyopiga kelele sana haswa ukiwa unaishi karibu na mto au mfereji halafu iwe ni msimu wa mvua patakuwa hapatoshi kwa sababu kelele zake zitakuwa siyo za kawaida, lakini katika msitu wa Amazon amegundulika chura mwenye ngozi ya kioo na ukimtazama unaona viungo vyote  unamwona kuanzia utumbo wake maini figo na kila kitu kinachopatikana tumboni mwake. Baada ya wanasayansi kumgundua chura huyo basi walimtungia jina na kumuita (Glass Frog)

Jesus Lizard

Katika msitu wa Amazon yupo kiumbe mwenye uwezo wa kutembea juu ya maji bila kuzama wala kuelea  ambaye anafahamika kwa jina la (Jesus Lizard)  wana sayansi wamempa jina hilo kwa kuwa kiumbe huyo ana  uwezo wa kutembea juu ya maji.

Boil River (Mto unaochemka)

Pia msitu wa Amazon una maajabu ya kutosha kama Boil River ambao ni mto unaochemsha maji na kuyafanya kuwa ya moto. Kuna baadhi ya vyura wenye viherehere hupenda kurukia ndani ya mto huo na kukutana na umauti. Baada ya wanasayansi kugundua mto huo wakaupa jina la Boil River na wameshindwa kujua nini kinachofanya maji ya mto huo kuwa ya moto.

Mto Amazon

Wanasayansi walichunguza na kugundua kuwa ndani ya msitu wa Amazon kuna mto mkubwa tena wa pili kwa ukubwa wenye kilometa 6,400. Baada ya kuendelea kufanya utafiti mwaka  2006  waligundua kuwa mto huo ulikuwa unatoa maji Amerika ya Kusini kupeleka Mashariki, lakini miaka 100 iliyopita Mto Amazon ulianza kupekeka maji kinyume nyume kiasi kwamba maji yanakuwa yanakwenda na kurudi yalikotokea.

Victoric Amazonika

Haya ni majani yaliyo na uwezo wa kufanya kazi kama mtubwi. Majani haya yanayopatikana katika masitu wa Amazon ambamo mtu anaweza akayatumia kusafiria na usizame. Majani haya yanafahamika kama Victoric Amazonika na huenea kama magugu ndani ya mito ya Amazon.

Ant Bullet (Siafu)

Katika kuhitimisha maajabu ya msitu wa Amazon kuna siafu wanaopatikana katika wanaojulikana katika jina la Ant Bullet ni siafu wakali na wanapatikana katika msitu huo na wamepewa jina hilo kwa kuwa wana uwezo wa kungata kwa kasi kwelikweli.

Taarifa kutoka mitandao wa Nat Geo Wild