Madai mahindi kuzuiwa kuingia Kenya, Bashe awatuliza wafanyabiashara

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amewasili mkoani Arusha kutatua kile kinachodaiwa kuwa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) imezuia magari ya mizigo yenye shehena ya mahindi kuingia nchini humo.

Arusha. Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amewasili mkoani Arusha kutatua kile kinachodaiwa kuwa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) imezuia magari ya mizigo yenye shehena ya mahindi kuingia nchini humo.

Taarifa ya zuio hilo imesambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia usiku wa kuamkia leo Jumamosi Machi 6, 2021 ikieleza kuwa magari yamekwama katika mpaka wa Namanga.

Akiwa katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Longido mkoani humo, Bashe ambaye ni mbunge wa Nzega Mjini (CCM) amesema Serikali ya Tanzania inachukulia kwa uzito unaostahili mazao yao kuzuiwa.

"Serikali inafutilia kwa karibu zuio hili niwahakikishie wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuwa serikali itaendelea kulinda maslahi yake," amesema Bashe.

Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi