Madaktari bingwa kutoka Marekani kuinua sekta afya Zanzibar

Muktasari:

  • Madaktari bingwa hao, wanategemewa kuisaidia sekta ya afya kuweka kitengo cha madaktari bingwa watakaofanya upasuaji katika hospitali mpya ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Lumumba.

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema ujio wa madaktari bingwa kutoka Marekani ni ishara njema kwa maendeleo ya sekta ya afya kisiwani humo.
Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Januari 25, 2023 Ikulu, Zanzibar alipozungumza na timu ya madaktari hao kutoka Marekani na Ubelgiji wakiongozwa na Professa Bruno Jvan Herendaw kutoka taasisi ya kimataifa ya International Society for Gynecologic Endoscopy (ISGE).
“Madaktari hao mbali ya kutoa mbinu za kibingwa pia watasaidi maeneo mbalimbali ikiwemo kutoa vifaa vya kisasa kwenye hospitali hiyo, utaalamu kwa madaktari wazawa na kuweka miundombinu sawa ya hospitali," amesema Dk Mwinyi
Madaktari bingwa hao, wanategemewa kuisaidia sekta ya afya kuweka kitengo cha madaktari bingwa watakaofanya upasuaji katika hospitali mpya ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Lumumba.
“Naanza kupata ishara ya hospitali hii itakavyokuwa bora na kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wote,” amesema.
Rais Mwinyi ametumia fursa hiyo kuipongeza timu hiyo ya madaktari kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwafikishia huduma za kisasa wananchi wake.
Kwa upande wake, Professa Bruno ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupata ushirikiano na watendaji mbalimbali waliokutana nao hususani wa Wizara ya afya.
Naye daktari bingwa wa wanawake kutoka hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Dk Sabra Salum Masoud amesema walifundishwa kuhusu upasuaji wa tumbo kwa wanawake kwa kutumia tundu dogo bila kuweka kovu.
Amesema mpaka sasa wamefanya upasuaji wanawake 17