Madiwani watoa maagizo kifuta jasho waliojeruhiwa na wanyamapori
Siha. Baraza la Madiwani Halmashauri Siha mkoani Kilimanjaro, limemtaka Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ofisa maliasili kwenda Wizara ya Maliasili ili kufahamu malipo ya kifuta jasho kwa watu waliopata majeraha kutoka kwa wanyamapori wilayani humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Diwani wa kata ya Orkolili Janathan Nasar kusema kwamba kwenye kata yake kuna mtu alijeruhiwa na mnyamapori na kupata majeraha ya kudumu lakini walipofuatilia kitengo cha wanyamapori hakuna majibu ya maana.
Wakizungumza kwenye Baraza la kawaida la Madiwani kuwasilisha taarifa za kata kilichofanyika ukumbi wa Halmshauri hiyo, wamemtaka Mkurungenzi Mtendaji pamoja na ofisa wanyamapori kwende wizarani kufuatilia kifuta jasho kwa wananchi walioumizwa.
"Ni kweli Kama baraza tumeshauri Mkurungenzi Mtendaji pamoja na ofisa wanyamapori waongozane kwenda wizarani kufahamu tatizo liko wapi kuhusu malipo kwa wananchi walioumizwa na wanyama hao ili kuondoa malalamiko kwa wananchi haoni," wamesema madiwani hao.
Nasari amesema wameshafutilia kwa muda mrefu kitengo cha maliasili hapo halmashauri ili kupata suluhisho la huyo mwananchi aliyepata majeraha lakini hakuna majibu.
Diwani wa Viti Maalumu, Jane Kimaro amesema hili jambo siyo sawa mtu anapata majeraha kutoka kwa wanyamapori hasa tembo unajiuguza fedha zote zinakwisha na kushindwa kuendesha familia.
Mwenyekiti wa Halmashauri Dancan Urasa, amesema ili Jambo Ofisi ya Mkurungenzi Mtendaji wanayoorodha ya wananchi hao kuanzia mwaka juzi, mwaka jana na mwaka huu, naomba mkurungenzi atoke na ofisa wanyapori waende Dodoma kwenye hizo ofisi ili waweze kufuatilia watu wetu haki yao.
Kaima Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Barnabas Mbwambo amesema kifuta jasho kipo lakini halmashauri haihusiki.
"Sisi ni waandaaji wa taarifa kwa ajili ya malipo ambayo ni Wizara ya Maliasili na taarifa za watu walioumizwa na wanyama hao zipo wizarani, niliongea na afisa wanyapori wa wilaya," amesema Mbwambo.