Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mafuriko yasababisha shule kufungwa Morogoro

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Ally Machele (mwenye suti nyeusi) akizungumza jambo na viongozi wa halmashauri hiyo na wilaya katika eneo litakalojengwa madarasa ya dharura ya Shule ya Msingi Juhudi katika Kata ya Lukobe mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa ametoa amri ya kufungwa kwa Shule ya Msingi Juhudi, baada ya kuzingirwa na maji ya mvua inayoendelea kunyesha.

Morogoro. Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa ametoa amri ya kufungwa kwa Shule ya Msingi Juhudi baada ya mvua zinazoendelea kunyesha kuhatarisha usalama wa wanafunzi wa shule hiyo, kufuatia maji kuzingira madarasa.

Pia Manispaa ya Morogoro imetenga Sh90 milioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya dharura eneo la Shule ya Sekondari Tushikamane Kata ya Lukobe mkoani hapa.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Februari Mosi,  2024 mkoani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Ally Machela amesema wametenga Sh90 milioni zitakazotumika katika ujenzi wa Shule ya Msingi Juhudi ambayo majengo yake yamekuwa yakikumbwa na  mafuriko.

Machela amesema tayari manispaa hiyo imewasilisha ombi mbele ya kamati ya fedha na uongozi ya halmashauri hiyo, ili kupata kibali cha ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo katika kipindi cha siku tano yawe yamekamilika.

“Kamati ya wataalamu wetu wanachosubiri kwa sasa ni kupata kibali kutoka Kamati ya usalama ya Wilaya ya Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya dharura,  lengo letu ndani ya siku tano ujenzi uwe umekamilika,” amesema Machela.

Machela amesema wanahitaji zaidi ya madarasa 20 ili kukidhi uhitaji kwa sababu Shule ya Msingi Juhudi ina wanafunzi zaidi ya 1,600.

Amesema pia  watajenga vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tano na kukamilisha maboma mawili yatakayotumiwa  na wanafunzi wa darasa la awali na ofisi ya walimu.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga amesema ameongoza wajumbe wa Kamati ya fedha na uongozi ya halmashauri kutembelea eneo la ujenzi wa shule hiyo na wameridhia kujengwa kwa shule hiyo katika eneo la Shule ya Sekondari Tushikamane.