Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magari yafurika Moshi, foleni yatisha

Msongamano wa magari

Muktasari:

Msongamano huo wa ongezeko la magari unalosababishwa na utamaduni wa wenyeji wa Mkoa Kilimanjaro, kurejea nyumbani.

Daniel Mjema, Mwananchi [email protected]

Moshi. Mji wa Moshi umekuwa na msongamano mkubwa wa magari katika barabara kuu ya kuingia mjini kutokea Dar es Salaam.

Msongamano huo wa ongezeko la magari unalosababishwa na utamaduni wa wenyeji wa Mkoa Kilimanjaro, kurejea nyumbani kutokea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Awali, ilitarajiwa kusingekuwapo na ongezeko hilo la wageni kwa mwaka huu, kutokana na ugumu wa maisha uliotokana na kupungua kwa mzunguko wa fedha mitaani.

Hata hivyo, juzi saa 12.00 jioni hadi saa 2.00 usiku, kuliibuka msongamano wa magari kuanzia eneo la Mbwaharuki hadi Magereza Barabara Kuu ya Dar es Salaam- Moshi.

Habari zaidi soma Gazeti Mwananchi