Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magonjwa ya moyo yazidi kutesa watoto

Muktasari:

Daktari wa magonjwa ya moyo kutoka Bugando, Bahati Kwandu alisema hospitali hiyo imefanikiwa kuwafanyia upasuaji watoto 215 kati ya 1,500 waliofikishwa hospitalini hapo kwa matibabu kati ya mwaka 2007 hadi mwaka huu.  

Mwanza. Asilimia 90 ya watoto kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wanaofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini hapa wanabainika kuwa na magonjwa ya moyo yanayohitaji upasuaji.

Daktari wa magonjwa ya moyo kutoka Bugando, Bahati Kwandu alisema hospitali hiyo imefanikiwa kuwafanyia upasuaji watoto 215 kati ya 1,500 waliofikishwa hospitalini hapo kwa matibabu kati ya mwaka 2007 hadi mwaka huu.  

Dk Kwandu aliyekuwa akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki, alitaja miongoni mwa sababu zinazokwamisha matibabu kwa baadhi ya watoto kuwa ni kucheleweshwa kufikishwa hospitali.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama ya moyo yameendelea kuwa tishio duniani. Tatizo hili linatarajiwa kuendelea hadi mwaka  2030,”  alisema Dk Kwandu.

Akizungumza suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo aliishauri Serikali kuanzisha kitengo cha huduma ya upasuaji wa moyo katika kila hospitali za rufaa za mikoa au za kanda ili kukabiliana na tatizo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliwashauri Watanzania kujiunga na mifuko ya bima ya afya ili kumudu gharama za matibabu ikiwamo ya upasuaji wa magonjwa ya moyo.

Alisema inakadiriwa kuwa ni asilimia 30 pekee ya Watanzania zaidi ya milioni 45 ndiyo waliojiunga na mifuko hiyo.