Magufuli aibukia Wizara ya Fedha, akosa maofisa ofisini
Muktasari:
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia leo, Rais Magufuli ameingia wizarani hapo kwa miguu, akitokea Ikulu ambapo baada ya kufika katika ofisi hizo, alipita chumba kwa chumba na kukuta wengi wameshaondoka.
Rais Dk John Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha na kuwakosa ofisini maofisa wengi katika wizara hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia leo, Rais Magufuli ameingia wizarani hapo kwa miguu, akitokea Ikulu ambapo baada ya kufika katika ofisi hizo, alipita chumba kwa chumba na kukuta wengi wameshaondoka.
Dk Magufuli ameapishwa jana asubuhi kuwa kiongozi mkuu wa nchi na ilipofika saa 7:20 mchana, aliingia Ikulu kuanza makazi mapya katika kipindi cha miaka mitano ambayo atawaongoza Watanzania.
Katika kampeni zake Dk Magufuli aliahidi kupambana na wazembe, mafisadi pamoja na wala rushwa.