Magufuli amtengua kigogo wa ardhi

Sunday January 17 2021
kigogo ardhi pic

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dk Steven Nindi.

By Herieth Makwetta

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dk Steven Justice Nindi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo Januari 17, 2021 na kwamba nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Dk Nindi aliteuliwa na Rais kushika wadhifa huo Julai 14 mwaka 2017, baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa muda.

Advertisement