Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama kulinda aina 3,000 ya wanyamapori waliopo hatarini

Muktasari:

  • Majangili wanapojitajirisha kupitia wanyamapori na misitu kiharamu wasiposhughulikiwa faida wanazozipata zinatumika katika vitu vingi vya haramu ikiwemo kufanya ugaidi.

Morogoro. Mahakama Kuu ya Tanzania inajipanga kusimamia na kulinda wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka nchini.

Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro, Latifa Mansoor amesema hayo Oktoba 9, 2023 mjini Morogoro kwa niaba ya Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapha Sayani wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya uendeshaji mashauri ya makosa ya wanyamapori na maliasili kwa majaji wa Mahakama Kuu, mahakimu, waendesha mashtaka na wapelelezi.

Jaji Mansoor amesema kuna aina 3,000 za wanayamapori waliopo hatarini kutoweka kati ya aina zaidi ya 10 milioni zilizopo nchini.

Amesema ili kuhakikisha wanayamapori hao wanalindwa elimu ya mashauri ya makosa kwa maofisa wa mahakama imekuwa ikitolewa na wameanza mwaka 2022 na itamalizika 2024.

Aidha amesema ipo haja ya kukabiliana na wimbi hilo kwa kutoa elimu ambapo pia inakadiriwa aina 16,000 za wanyamapori wapo hatarini kutoweka kidunia.

Hivyo amesema kama nchi wana mipango ya kulinda wanyamapori kwa kusimamia na kuhifadhi mazingira, uasili na biashara ya kimataifa.

"Kama itatokea jangili anamdhuru mnyamapori yoyote anayekwenda kupotea mafunzo haya yatasaidia kushughulikiwa na kuwa mfano kwa majangili wengine kutojaribu kuharibu," amesema.


Hata hivyo amesema Serikali inapigana na rushwa na kwamba ingawa majangili wataonekana wanauwezo wa kifedha kutokana na kuuza rasilimali wataagiza kutolewa adhabu kali kwao.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation ambao ndio wafadhili, Samson Kasala amesema wana jitihada za kulinda na kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na maliasili nchini ambapo ushirikiano na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) utasaidia namna ya kushughulikia kesi za wanyamapori kwa ufanisi zaidi.

Wakili wa Serikali Ofisi ya Mashtaka Taifa Mkoa wa Pwani, Clarence Mhoja amesema mafunzo hayo yatawasaidia kufikia hatua nzuri ya kupeleka jalada mahakamani hapo wenzao wa ukamataji na upelelezi wanapotekeleza kazi zao kwa mujibu wa sheria.