Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa ataka ubunifu kuondoa msongamano Tunduma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Muktasari:

  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa azitaka Halmashauri kutafuta eneo la kujenga maegesho ya malori ya mizigo, Vwawa ili kupunguza msongamano Tunduma.

Songwe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, kubuni mradi wa maegesho ya malori ili kupunguza msongamano uliopo katika Mji wa Tunduma.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 24, 2023 aliposimama kuwasalimia wananchi wa  Jimbo la Vwawa ikiwa ni siku  ya pili ya ziara yake  Mkoa wa Songwe katika Wilaya ya Ileje na Mbozi .

Amesema umefika wakati wataalamu watumie uwezo wao wote kufanya Mji wa Vwawa kuwa pumulio la msongamano uliopo Tunduma hivi sasa.

“Nimewaagiza wataalamu kutafuta eneo ambalo wanaweza kujenga maegesho ili madereva wa malori waweze kupumzika wakati wanasubiri kuvuka mpaka wa Tunduma sambamba ujenzi wa nyumba za kutosha za kulala wageni zitakazo chochea mapato ya Serikali.

Awali, Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga, ameomba kujengwa stendi kubwa ya kisasa, soko la mazao la kimataifa ili wakulima waweze kulitumia kuuza mazao yao kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi badala ya kuwaacha waende hadi mashambani.