Makandarasi wanaochelewesha kazi wapewa onyo

Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka, akiwa katika moja ya ziara yake kutembea miradi ya ujenzi wa elimu na Afya wilayani humo
Siha. Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Christopher Timbuka amesema atawachukulia hatua makandarasi wa ujenzi watakaoshindwa kumaliza kazi kwa mujibua wa mkataba unavyowataka.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake yenye lengo kutembea miradi hiyo ikiwamo ya elimu na afya inayotekelezwa wilayani humo inakamilika kwa wakati ambapo baadhi aliikuta ikisuasua bila sababu za msingi.
Akizungumza akiwa Kijiji cha Ormelili kuangalia ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Ormelili, amesema hatasita kuwachulia hatua wanaokwamisha kumaliza ujenzi kwa sababu za uzembe wakati fedha za miradi zipo.
"Ni kweli fedha zipo, uzembe unatoka wapi, kuna shule tatu za sekondari tumefika tumekuta ujenzi unasuasua. Tumekuta vibarua peke yao mafundi hawapo kazini, tumewapa angalizo,"amesema Timbuka.
Timbuka amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameleta miradi ya kutosha wilayani humo na kwamba mwaka huu imeletwa miradi 30 ambayo tunatembelea sehemu mbalimbali ndani ya wilaya.
Amesema kuna miradi ya shule ambayo inatakiwa kukamilika Septemba mwaka huu, tunayo miradi ya afya inatakiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Pia, kuna miradi mingine ya elimu na afya ambayo mwishoni mwa Desemba hii ni pamoja na Shule ya Wasichana ya Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Chuo cha Ufundi Veta inatakiwa kukamilika.
Kwa hiyo nitumie nafasi hii kuwasihi sana wote walishika mikataba au wakandarasi wafanye kazi kwa mujibu wa mkataba wao, kipindi hiki cha mwisho tutakuwa tunapita mara kwa mara wahandisi wabaki kwenye maeneo yao ili waweze kutatua changamoto.
Naomi Swai kwa niaba ya mkurungenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, amesema kukamilika kwa miradi hiyo ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na pia mazingira ya utuaji huduma za afya.
Amesema, fedha ni nyingi zimetumwa katika halmshauri hii mfano sekta ya Afya zaidi ya Sh2 bilioni sekta ya elimu zaidi ya sh7 bilioni.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo Wilfred Mosi amesema Serikali wilayani humo inachofanya kutembea miradi imelizike kwa wakati ni kutekeleza ilani ya chama hicho ili huduma iweze kuanza kwa walengwa ni jambo zuri.