Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda, Lemutuz kortin kwa uporaji gari

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Muktasari:

  • Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na William Malecela, maarufu Lemutuz wamefunguliwa kesi mahakamani kwa tuhuma za uporaji gari aina ya Range Rover.

  

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na William Malecela, maarufu Lemutuz wamefunguliwa kesi mahakamani kwa tuhuma za uporaji gari aina ya Range Rover.

Makonda na Lemutuz, ambaye ni mwanamitandao anayemiliki blogu ya Lemutuz, wamefunguliwa kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mfanyabiashara Patrick Christopher Kamwelwe.

Katika madai yake, mfanyabiashara huyo anataka alipwe fidia ya zaidi Sh240 milioni ambazo ni gharama za kodi thamani ya gari hilo la kifahari.

Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na wakili wa mfanyabiashara huyo, Kung’e Wabeya, kesi hiyo ya madai namba 234 ya mwaka 2022 imepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Oktoba 13, mwaka huu, saa 7:00 mchana.

Kufuatia kesi hiyo, tayari mahakama hiyo imetoa taarifa kwa wadaiwa ikiwajulisha kufunguliwa kesi hiyo mahakamani hapo na kuwataka wawasilishe mahakamani utetezi wao wa maandishi ndani ya siku 21, tangu tarehe ya kupokea taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Septemba 23 mwaka huu ambayo Mwananchi limeiona nakala yake, ikiwa watashindwa kuwasilisha mahakamani utetezi wao huo wa maandishi ndani ya muda huo ulioainishwa, basi mahakama itaweza kutoa hukumu dhidi yao.

Wakili Wabeya hakutaka kueleza zaidi kuhusiana na kesi hiyo, akisema kwa sasa yeye hawezi kuongea zaidi, isipokuwa mteja wake mwenyewe ndiye anaweza kuizungumzia, lakini akaahidi yeye atazungumza zaidi Oktoba 13 baada ya kesi hiyo kutajwa.

Kamwelwe ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani hakuweza kupatikana jana, lakini kabla ya kufungua kesi hiyo aliwahi kunukuliwa na gazeti moja nchini, na kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akitoa malalamiko yake ya kudai kuporwa gari hilo.