Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malisa afikishwa mahakamani Kilimanjaro, kusomewa mashtaka

Mwanaharakati, Godlisten Malisa, akiwa na mawakili wake, Dickson Matata na Hekima Mwasipu katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi. Picha Omben Daniel

Muktasari:

  • Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusafirishwa hadi mkoani Kilimanjaro akikabiliwa na tuhuma tatu.

Moshi. Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa leo Julai 18, 2024 amefikishwa mahakamani akisubiri kusomewa mashitaka yake likiwamo la uchochezi yanayomkabili.

Hata hivyo, bado haijafahamika Malisa atapandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi au Mahakama ya Wilaya Moshi kwa kuwa mahakama zote zinatumia jengo moja.

Tayari mawakili wake, Hekima Mwasipu na Dickson Matata wamefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Wengine waliopo katika viunga vya mahakama hiyo ni wafanyakazi wa taasisi yake, akiwemo James Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro na marafiki zake wa karibu.

Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na alisafirishwa hadi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuja kujibu tuhuma zinazomkabili.

Inaelezwa kuwa Malisa anakabiliwa na tuhuma tatu ikiwamo ya kuchapisha taarifa za uchochezi kuhusu mauaji ya Beatrice Minja, mkazi wa Rombo anayedaiwa kuuliwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Paul Tarimo na tukio la mwanafunzi anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa mjini Moshi.

Tuhuma nyingine ni kutoa taarifa bila kibali kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusu walimu waliokuwa wakisahihisha mitihani ya kidato cha nne Januari, mwaka huu kutolipwa posho zao.

Kabla ya leo, mwanaharakati baada ya kurejeshwa Moshi, aliachiliwa kwa dhamana na alitakiwa kuripoti katika Ofisi za Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro (RCO).

Godlisten Malisa akiwa na wenzake katika viunga vya mahakamani Moshi akisuburi kusomewa mashitaka mbalimbali ikiwemo ya uchochezi yanayomkabili. Picha na Omben Daniel

Mara ya mwisho kuripoti katika ofisi hizo ilikuwa Julai 11, 2024 ikiwa ni mara ya tatu kufanya hivyo tangu alipopatiwa dhamana Juni 8, 2024.