Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama ajifungua watoto wanne kwa mpigo Dar

Mama Mapacha

Muktasari:

Mama huyo amesema hakutarajia kujifungua idadi hiyo ya watoto lakini anamshukuru Mungu kwa kuwa atakuwa na watoto watano sasa.

Dar es Salaam. Ofisa Tarafa wa Kibamba, wilayani Ubungo, Beatrice Mbawala amejifungua watoto wanne kwa mpigo katika Hospitali ya Agha Khan, jijini hapa.

Beatrice amejifungua watoto hao wakiwa njiti mwezi mmoja uliopita.

Akizungumza hospitalini hapo, leo Machi 3, baba wa watoto hao, Julius Mbawalla amesema familia yake ina furaha kupokea watoto wanne na kwamba jukumu lake kubwa ni kuhakikisha mkewe anapata huduma muhimu ili aweze kumudu kuwanyonyesha.

Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Agha Khan, Dk Mariam Mgonja amesema afya za watoto zimeimarika na tayari wameruhusiwa kwenda nyumbani.