Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama amjeruhi mwanaye kwa kumchoma na panga

Mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Ubetu aliyeunguzwa na panga lenye moto na mama yake mzazi.

Muktasari:

Severa Tesha(32) mkazi wa Kijiji cha Ubetu, Kata ya Ubetu Kahe, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro amemchoma mwanaye kwa panga lenye moto sehemu za mapajani na kumsababishia majeraha na maumivu.

Rombo. Severa Tesha (32) mkazi wa Kijiji cha Ubetu, Kata ya Ubetu Kahe, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro amemchoma mwanaye kwa panga lenye moto sehemu za mapajani na kumsababishia majeraha na maumivu makali.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi  Ubetu amefanyiwa ukatili huo na mama yake mzazi kwa madai ya  kutoosha vyombo ambavyo aliagizwa avioshe.
Mpaka sasa mwanafunzi huyo ameshindwa kwenda shule kutokana na majeraha.
Akizungumzia tukio hilo  Mei 11,2022  Mwalimu wa malezi wa shule hiyo, Notibruda Massawe amesema baada ya kufanyika tukio hilo  mama mzazi wa mwanafunzi huyo alipiga simu shuleni akidai mwanaye huyo anajipu hawezi kutembea.
"Huyu mama alitoa taarifa shuleni kwamba mwanaye ana jiipu hawezi kutembea kufika shuleni,lakini baadaye ndugu zake walipiga simu kwamba huyu mtoto amechomwa na mama yake mzazi," amesema.
"Na sisi kwa kujiridhisha tulienda kumuona na tumekuta amejeruhiwa mapaja yote mawili na hawezi kutembea lakini kwa sasa anaendelea na matibabu," amesema.
Naye msaidizi wa masuala ya Kisheria Wilaya ya Rombo, Remmy Shirima amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika nyumbani kwa mama huyo ambapo baada ya kuona mtoto huyo amejeruhiwa  alitoa taarifa polisi na mama huyo  alikamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Usseri.
Mpaka sasa mama huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo.