Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama aua watoto wake kwa sumu, kisa ugumu wa maisha

Muktasari:

  • Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha


Mwanza. Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.

Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 2, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.

Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.

Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.

“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe