Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamba wawili wauawa Ziwa Victoria

Wananchi wa Kijiji cha Kanyala Kata ya Bulyaheke wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wakichuna mamba mara baaada ya kuvunwa na Tawa. Picha na Daniel Makaka

Muktasari:

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) imetumia siku 14 kuua mamba wawili Ziwa Victoria waliokuwa wakisumbua wananchi wa visiwa vya Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Buchosa. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) imetumia siku 14 kuua mamba wawili Ziwa Victoria waliokuwa wakisumbua wananchi wa visiwa vya Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 29, 2023 katika kijiji cha Kanyara baada ya kuvuna mamba mmoja, Ofisa Wanyamapori Msaidizi daraja la II, Moris Mapima amesema doria lilianza Agost 17 Kijiji cha Izindabo Kata ya Lugata na kumalizika Agosti 28 katika Kijiji cha Kanyala Kata ya Bulyaheke Halmashauri ya Buchosa.

Amepongeza ushirikiano walioupata toka kwa wananchi na viongozi wa maeneo hayo walipokuwa wakifanya doria hali iliyopelekea kufanikisha zoezi hilo.

“Haikuwa kazi rahisi lakini kutokana na ushirikiano wa viongozi na wananchi tulifanikisha zoezi,”amesema Mapima

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kanyala, Gacha Paul ameiomba Tawa kufika mapema maeneo yenye mamba pale wanapopewa taarifa ili kuwasaidia wananchi na kuepusha madhara ikiwemo vifo na majeruha.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Jumanne John amesema kutokana na mamba huyu kuuawa watapata nafuu kwakuwa aliwasumbua akiomba doria ziendelee ili mamba wengine waendelee kuvunwa.