Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 pasua kichwa Januari

Muktasari:

Baada ya kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, vichwa vya watu wengi sasa vimeelemewa na mawazo kuhusu gharama za watakazokabiliana nazo mwanzoni mwa mwaka.

Dar es Salaam. Baada ya kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, vichwa vya watu wengi sasa vimeelemewa na mawazo kuhusu gharama za watakazokabiliana nazo mwanzoni mwa mwaka.

Januari au ‘njaanuari’ kama inavyofahamika kwa wengi ni mwezi ambao unazungumziwa kuwa mgumu zaidi kifedha kuliko mingine yote kutokana na wengi kutikiswa na mahitaji muhimu yapatayo 10 hivi.

Mambo hayo ni kodi ya nyumba kwa wanaoishi kwenye nyumba za kupanga, ada za shule kulingana na watoto waliopo katika familia pamoja na mahitaji ya shule ya watoto zikiwamo gharama za usafiri kwa wale wanaosoma mi koani.

Hayo yakifanyika bado bili za maji, umeme na mahitaji ya vyakula, gesi au mkaa yanaendelea kuwapo kama kawaida. Gharama hizi zitaendelea na kuongeza uzito wa majukumu ya Januari.

Kwa wafanyabiashara mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwani kuna pango la eneo la biashara na kodi nyingine zinazopaswa kulipwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bila kusahau marejesho ya mikopo kwenye taasisi za fedha.

Wanaomiliki magari nao wana mzigo wa gharama zikiwamo bima, mafuta na marekebisho ya hapa na pale.

Mambo hayo yote yanasababisha maumivu ya kichwa kwa watu wengi na kuufanya Januari kuwa gumzo vijiweni, mitandaoni na kwenye mikusanyiko ya watu kutokana na machungu yake.

Gazeti hili limezungumza na watu wanaoguswa na mambo hayo pamoja na watalaamu wa uchumi na mwanasaikolojia walioshauri namna ya kukabiliana na mzigo wa Januari.

Mkazi wa Kigamboni na mfanyabiashara wa mitumba, Nelson Mrisho alisema mzigo alionao Januari unamfanya atumie muda mwingi kuwaza ni wapi atapata fedha za kutosha mahitaji yake.

“Tarehe 15 natakiwa kulipa kodi ya nyumba Sh1.8 milioni na mtoto wangu wa kwanza anaingia kidato cha kwanza inatakiwa ada na mahitaji mengine mengi. Hapo kuna bili ya maji, umeme, malipo ya msichana wa kazi nikifikiria hayo yote kichwa kinawaka,” alisema Mrisho.

Naye Merina Joseph, mkazi wa Mtoni Kijichi alisema ni kawaida kwake kila inapofika Januari mambo kuwa magumu kutokana na majukumu yanayokabili.

“Kwangu miaka yote Januari ni ngumu ingawa mwaka huu kuna mabadiliko kidogo. Sasa hivi sikai kwenye nyumba ya kupanga hivyo sidaiwi kodi lakini kuna mtoto namsomesha amefaulu kwenda kidato cha kwanza hayo mahitaji ni shughuli nyingine.

“Sasa nipate vitu vyote hivyo, nina mkopo Vicoba natakiwa kulipa marejesho, nilichukua mkopo mwingine benki kwa ajili ya ujenzi wa nyumba niliyohamia pamoja na biashara huko nako natakiwa kupeleka marejesho basi ni changamoto

“Shuleni kuna fomu tumepewa inatakiwa kurudishwa na Sh15, 000 hapo mtoto anatakiwa akafanyiwe vipimo hospitali Sh20, 000 natakiwa kulipa hela ya nguo za michezo Sh25,000 hapo bado sare za shule, sweta, viatu vya darasani, raba na madaftari nimeambiwa 10 haya ni Sh25,000 nikienda duka la jumla,” alisema

Wakati mkazi wa Mtoni Kijichi, Barnaba Lucas, baba wa watoto wanne alisema kama isingekuwa kuendesha mambo yake kwa bajeti, ingekuwa vigumu kwake kusomesha watoto.

“Januari ni mwezi unaoumiza, usipokuwa makini unaweza kuuza hata vitu vya ndani ili ulipe ada za watoto. “Bajeti ndiyo kila kitu, unaangalia nini kifanyike kwa wakati gani ili kuondoa matumizi yasiyo ya lazima. Hata ukiwa unaingiza pesa nyingi kama hauna mipango, utaumia,” alisema.