Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamia wajitokeza Nida Dar, walalamikia mitandao ya simu kukwamisha usajili wa laini

Muktasari:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Jumatatu Saa 5.59 usiku, itazifungia laini zote ambazo zitakuwa hazijasajiliwa kwa alama za vidole. Ili laini isajiliwe lazima muhusika awe na kitambulisho au namba ya taifa ambayo kupatikana kwake imekuwa changamoto kubwa. Pia, mitandao kwa baadhi ya kampuni za simu imekuwa kikwazo kwani licha ya kuwa na kitambulisho cha taifa au namba unaweza ukashindwa kujisajili.

Dar es Salaam. Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufungwa kwa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole, mamia ya wananchi wamejitokeza katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) wilaya ya Ilala Dar es Salaam huku wakilalamikia kasi ndogo ya utoaji huduma.

Nje ya ofisi za Nida zilizopo Ukonga, usajili wa laini za simu pia unaendelea huku mawakala nao wakilalamikia tatizo la mtandao, jambo linalokwamisha usajili wa laini za simu kwa haraka na muda mfupi.

Mwananchi limeshuhudia baadhi ya watu ambao wamefanikiwa kupata namba zao za kitambulisho kabla ya ukomo wa muda kufika leo Jumatatu Januari 20, 2020 saa 5.59 usiku, wakiwa na furaha kwa kukamilisha mchakato huo.

 

"Aisee nimepiga kambi hapa tangu saa moja, watu walikuwa wengi lakini nashukuru leo nimekamilisha. Ingawa bado sijapata kitambulisho lakini angalau naweza kusajili laini yangu. Changamoto hapa ni kasi ndogo ya watendaji wa Nida," amesema Fadhili Mohammed, mkazi wa Majumba Sita.

 

Kwa upande wake, mkazi wa Gongo la Mboto, Martha Haonga amesema bado hajafanikiwa kupata namba ya kitambulisho chake lakini ataendelea kusubiri aone kama atafanikiwa.

 

"Mi hata sielewi kama nitaipata hiyo namba leo au la! Wakinifungia laini zangu, basi, nitaendelea kuja mpaka nipate hiyo namba. Nimeacha shughuli zangu kwa ajili ya kushughulikia hili suala," amesema mwanamke huyo.

 

Mmoja wa mawakala wanaosajili laini za simu, Ombeni Mwanjisi amesema usajili unafanyika kama kawaida lakini wanakabiliwa na changamoto ya mtandao ambao unakuja na kuondoka.

 

"Mtandao sio mzuri, tunatumia muda mrefu kusajili mtu mmoja. Baadhi ya kampuni za simu kama Halotel, mtandao uko vizuri lakini mingine lazima usubiri," amesema wakala huyo wakati akiendelea na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mkazi wa Tabata Dar es Salaam, Ibrahim Abdallah amesema ameshindwa kusajili laini yake kutokana na mtandao wa kampuni ya simu kuwa chini.

“Mimi jana nimeshinda kwa wakala wa mtandao wa Vodacom toka asubuhi hadi jioni lakini sikusajili kwa sababu mtandao ukiwa unasumbua na leo nimekwenda hali ni ile ile kwa hiyo Serikali inapaswa kuliona hili kwani si makosa yangu ila ni mtandao,” amesema