Manispaa yawageuzia kibao wafanyabiashara

Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Picha ya maktaba

Muktasari:

Uamuzi huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa  hiyo, John Wanga baada ya kufunga vibanda 164 kati ya 213.

Mwanza. Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imewapa saa 48 wafanyabiashara waliopanga vibanda Kituo cha Mabasi cha Buzuruga, kulipa Sh94.4 milioni za malimbikizo ya kodi ya pango.

Uamuzi huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa  hiyo, John Wanga baada ya kufunga vibanda 164 kati ya 213.

Wanga alisema manispaa hiyo hiyo imetoa muda huo kuanzia jana, ikiwa ni malipo ya pango kwa miezi mitatu.

 Mmoja wa wapangaji katika vibanda hivyo, Daud Wilson alipongeza uamuzi wa manispaa hiyo kupiga marufuku wenye zabuni kupangisha watu wengine, kwani utapunguza bei wanazotozwa wamiliki hao kulinganisha na inayolipwa manispaa.