Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masola: Ni fedheha kuagiza sukari na mafuta nje ya nchi

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, (NBS) Daniel Masola

Muktasari:

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, (NBS) Daniel Masola amesema ni fedheha kwa taifa kuagiza sukari na mafuta ya kula nje wakati kuna uwezekano wa kuzalisha bidhaa hizo ndani ya nchi.

Mbeya. Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, (NBS) Daniel Masola amesema ni fedheha kwa taifa kuagiza sukari na mafuta ya kula nje ya nchi wakati kuna uwezekano wa kuzalisha bidhaa hizo ndani ya nchi.

 Akizungumza kwenye Kongamano la Shamba Dalasa lililoandaliwa na Kampuni Mwananchi Communications Ltd (MCL) kupitia Farm Clinic leo Agosti 4, 2022, Masola amesema bidhaa hizo zinapoagizwa nje ya nchi zinasababisha kuzalisha ajira huko badala ya ndani.

Amesema ili kufanikiwa katika kuzalisha bidhaa za kilimo za kutosha ndani ya nchi, takwimu za idadi ya watu na shughuli wanazofanya ni muhimu katika maendeleo ya sekta ya kilomo.

Ameongeza kuwa katika Sensa ya Watu na Makazi, wanakusudia kukusanya taarifa za kilimo, uvuvi hasa ufugaji wa samaki na mifugo.

 “Tutakusanya takwimu za mashamba ya miti, taarifa za kaya zinazojihusisha na ukulima wa miti na umilikaji wa mashamba,” amesema Masola.

Alitaja eneo jingine muhimu wanalotarajia kulifanyia kazi kwenye sensa hiyo ni ufugaji wa nyuki ambao kwa sasa ni shughuli ya kiuchumi yenye fursa kubwa ya kuliingizia nchi fedha.

“Kama huna takwimu za kutosha hata hiyo Trilioni moja tunayoona kubwa ukiwa na takwimu sahihi unaweza kuta ni ndogo,” amesema Masola.

Amesema ukiwa na takwimu sahihi ni  rahisi kuomba bajeti ya kutosha kwenye sekta ya kilimo ili kufikia ajenda ya 10/30.

Amefafanua kuwa kukiwa na takwimu za kilimo ni rahisi kujenga hoja na kupata raslimali zinazotekeleza kufikia mipango inayowekwa.