Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili wa Serikali watahadharishwa na rushwa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima akifungua mafunzo ya makosa ya mtandao kwa mawakili wa serikali mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda.

Muktasari:

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhani Kailima amewataka mawakili wa Serikali kujifunza Sheria ya Makosa ya Mitandao ili kukabiliana na uhalifu utokanao wa teknolojia ya mawasiliano.

Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima amewataka mawakili wa Serikali na waendesha mashtaka kujiepusha na vitendo vya rushwa baada ya kupata mafunzo ya makosa ya mtandao.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya makosa ya mtandao kwa mawakili wa serikali mkoani Morogoro leo Machi 9, Kailuma amesema kuwa tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961 kumekuwa na mabadiliko ya kimfumo yaliyogusa sera, siasa na uchumi.


Amesema mabadiliko hayo yamesababisha marekebisho ya vifungu vya Katiba, sheria na kanuni na kusababisha, akitoa mfano wa Sheria ya Makosa ya Mitandao ya 2015, iliyotungwa ili kuendana na kasi ya teknolojia ya mawasiliano duniani na makossa yatokanayo na matumizi yake.

“Matukio ya kimtandao yalianza kushamiri na ilipelekea kutoa mwanya au udhaifu katika mifumo na kusababisha wahalifu kufanya uhalifu. Kabla ya sheria hiyo ilikuwa vigumu kuwadhibiti wahalifu hao pale wanapotenda makosa kwa njia ya mtandao,” amesema Kailuma.

Ametaja vifaa wezeshi vya mawasiliano vya elekroniki kama simu, laptop akisema vinatumika kutenda makossa hayo, ikiwa pamoja na kusambaza picha za ngono, taarifa za uongo, vitendo alivyosema havikuwepo miongo miwili iliyopita.

Amewataka waendesha mashtaka wa serikali kujiimarisha katika maeneo ya sayansi na teknolojia ili kubaliana na uhalifu huo ukiwemo ugaidi, rushwa, dawa za kulevya, utakataishaji wa fedha haramu na usafirishaji haramu wa binadamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mashtaka wa serikali (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema mafunzo hayo yamewezeshwa na wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia Kamati ya Kitaifa ya Kusimamia Utatuzi wa Matumizi Mabaya ya Huduma na Bidhaa za Mawasiliano.

Amsema kwa takribani miongo miwili iliyopita makosa ya mtandao Tanzania na dunia kiujumla yamekithiri kwa kasi kwa kuchangiwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia habari na mawasiliano na nchi hii inayo nafasi ya kushughulikia changamoto zake.

“Mawakili wa serikali wamnaopata haya mafunzo tujitathimini na mchango huu mkubwa tuliopatiwa na wenzetu wa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na tuna zaidi ya miaka 10 toka utungwaji wa sheria mbalimbali za makosa ya mtandao nay ale yanayoendayo nayo kutumia mafunzo hayo kujijenga zaidi katika utendaji kazi wa kila siku,” amesema Mkurugenzi Mwakitalu.