Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili wabishania rejista ya mahabusu kesi kina Mbowe

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  •  Shahidi wa kwanza katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ametoa ushahidi leo Jumatano Novemba 10, 2021 huku yakitokea mabishano ya kisheria kati ya Jamhuri na upande wa utetezi.


Dar es Salaam. Shahidi wa kwanza katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ametoa ushahidi leo Jumatano Novemba 10, 2021 huku yakitokea mabishano ya kisheria kati ya Jamhuri na upande wa utetezi.

Kesi hii ndogo inatokana na pingamizi la mawakili wa utetezi kupinga kupokewa maelezo ya onyo yanayodaiwa kuwa ya mshtakiwa wa tatu katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi.

Upande wa Mashtaka wanaanza kujibu hoja za pingamizi la mawakili wa utetezo kuhusu kitabu cha Kumbukumbu za mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar.

Wakili Abdallah Chavula: Baada ya kusikiliza hoja za utetezi, hatukubaliani nao kwa sababu, hoja ya  kwanza Mtobesya ameleeza kuwa shahidi ameshindwa kuweka msingi kwani hajaieleza mahakama mara ya mwisho alipoiona nyaraka leo hii imefika vipi mokononi mwake na kwamba competence ya witness inaendelea pale shahidi atakapo- authenticate document (atakaonesha kujihusisha na nyaraka).

Wakili Abdallah Chavula: Katika ukurasa wa saba wa uamuzi wa shauri walilolirejea, kuna namna tatu za ku-authenticate kilelezo. Vigezo vilivyowekwa kwenye shauri hili havitumiki kwenye kielelezo ambacho ni nyaraka, kwenye kesi hii ilizungumzia kielelezo ambacho ni gari, tofauti na kilichopo kwenye shauri hili.

Wakili Abdallah Chavula: Msingi wa wenzetu umejikita katika competence ya witness (Shahidi kuwa na mamlaka au haki juu ya jambo au ).

Wakili Chavula anaielekeza mahakama kwenye shauri moja lililowahi kuamuriwa na Mahakama ya Rufaa lenye mazingira yanayofafana.

Wakili Chavula: Hapa mahakama nayo ilikutana na hali Kama hii tofauti ni kwamba katika shauri hilo lilikuwa linahusika kupokea kielelezo cha ushahidi na hapa sisi linahusu kielelezo cha utambuzi lakini Kanuni za upokeaji ni zilezile.

Katika shauri la DDP (Mkurugenzi wa Mashtaka) dhidi ya Mohamed ambalo upande wa utetezi unalirejea, Mahakama ya Rufaa  miongoni mwa mambo mengine ni knowledge

Wakili Chavula: Subject matter yetu ( jambo la msingi) katika jambo hili ni kielelezo cha Agosti 7, 2020, saa 2 asubuhi.

Wakili Chavula: Shahidi ameeleza alifika chumba cha mashtaka Central Police Dar kwa lengo la kupatiwa ntuhumiwa na akaweka saini kwenye kielelezo anachotaka kukitoa, akahojia shahidi utakitambuaje?

Wakili Chavula: Shahidi akasema kwa saini yangu, akaendelea akasema majina ya mtuhumiwa, akaenda akasema kumbukumbu  ya shauri lililoko hapo kituoni na mwisho akasema hayo yote utayakuta kwenye entry ya Agosti 7.2020

Mheshimiwa Jaji kitu gani kingine atafanya? Hayo ndio ya muhimu.

Wakili Chavula: Mheshimiwa Jaji nikihusianisha na haya yaliyosemwa kwenye mashauri haya mawili na shauri hili, shahidi wetu ana information na knowlege ya hizo entry za tarehe 7 ,mwezi wa 8, 2020.

Wakili Chavula: Wenzetu wamekwenda mbali na kusema suala la chain of custody (mnyororo wa utunzaji vielelezo) lakini hakusema kwa vigezo gani na hakutoa hata kifungu cha Sheria.

Katika shauri la Jamhuri dhidi ya Charles Abel maarufu kama Gasilabo ambalo tumekuletea, pia kilichokuwa kikibishaniwa ni nyaraka na mahakama ilisema chain of custody kinakuwa mwishoni mwa shauri

Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji nianze kwa kusema nayaunga mkono yote hayo ambayo wakili Chavula ameya submit.

Wakili wa Serikali Hilla:  Bila kuathiri hayo yote nami naongeza kidogo. Shahidi aliyeko kizimbani wakati ana- testify (ametoa ushahidi) ameileza mahakama kuwa alimfikisha mtuhumiwa Kituo cha Kati Dar na wakaingizwa mahabusu.

Wakili wa Serikali Hilla: Mheshimiwa hatuna Dar nyingine, hatuna kituo cha kati kingine Dar ambacho mahakama inaweza ikafikiria ni tofauti na alichokitaja shahidi.

Wakili wa Serikali Hilla: Amesema Agosti 7, 2020 alikwenda CRO Charge room office- (chumba cha mashtaka) akamto mtuhumiwa na akasaini nyaraka hiyo. Huo ni ushahidi tosha kuwa shahidi ameweka foundation (msingi)

Wakili wa Serikali Hilla: Kuhusu hoja ya Kibatala kwamba kielelezo kilitakiwa kitolewe masijala na si  kama tulivyokiomba.

Wakili wa Serikali Hilla:  Kwenye hili Mheshimiwa wenzetu hawako sawa. Mahakama yako Tukufu haijaelezwa ni kwa sheria gani na haijaelezwa ni kwa namna gani washtakiwa wameathiriwa

Wakili wa Serikali Hilla: Kibatala aliieleza mahakama kuwa trial within trial in respect ( kuhusiana na ) Adamu ni tofauti na mambo yake yaliisha.

Wakili wa Serikali Hilla:  Shauri hilo la Adamu ni shauri dogo ndani ya shauri hili na good thing ni kwamba mahakama haijawahi kutoa order ya ku- dispose kielelezo hicho. Kwa hiyo hatuja violate sheria na taratibu zozote. Ukizipima hizi hoja haziwezi kuzuia upokewaji wa nyaraka hii, hazina uzito huo.

Wakili wa Serikali Hilla:  Pasipo kuichosha mahakama yako Tukufu tunaomba mahakama yako iyatupilie mbali mapingamizi haya na nyaraka ambayo shahidi ameitambua tuendelee na shauri hili.

Wakili Jeremiah Mtobesya anasimama Tena akisisitiza hoja zake za awali na anasema kwamba anaongeza kidogo akisema “Authentication ni zoezi linalofanywa na shahidi na ndio maana kwenye hilo shauri la DPP dhidi ya Sharifu inasema ni shahidi anapaswa ku-authenticate exhibit na si chenyewe”

Wakili Mtosbeya: Kuhusu kiini Cha objection yetu nimemsikia wakili wa Serikali ni kama kwamba  kinachotakiwa kuwa authenticate ni entry na indictment bila shaka hii ni misguided submission, kinachopaswa kuwa authenticated ni document

Wakili Mtosbeya: Kwa hiyo bado tuna-isist kwamba shahidi huyo hajaweza ku- authenticate document hiyo either kwa unique features or chain of custody.

Wakili Mtosbeya: Kwanza mheshimiwa Jaji siyo kitu cha ajabu yeye anayeomba kui- tender (kuiwasilisha mahakamani) angeweza kusema walau kuwa ameitoa wapi na iko katika hali gani.

Wakili Mtosbeya: Hatukatai ufahamu ( wa kielelezo) ni suala la msingi lakini kwenye kesi hii mazingira ni tofauti na ukisoma katika shauri hilo la Gasilabo ( kesi rejea iliyiwasilishwa) kulikuwa na taarifa za kutosha na Mahakama ya Rufani ilikwenda mbali ikasema kulikuwa na unique features.

Kwa hiyo tunakubali na suala la knowledge lakini distinguish (tunatofautisha) mazingira hayo.

Wakili Mtosbeya: Shahidi hajaonesha unique features kwenye hiyo document, hatukatai Police Central Dar ni moja lakini bado hakuna unique features.

Kanuni za upokeaji kielelezo iwe kwa ushahidi au kwa utambuzi ni zilezile na hivyo tunasisisitiza nyaraka hii isipokewe for identification purpose.

Wakili Paul Kaunda kwa niaba ya mshtakiwa wa pili, Adam Kasekwa.

Wakili Kaunda: Shahidi aliyeko kizimbani hajaiambia mahakama nini kiliendelea kuanzia Agosti 7,2020 mpaka Sasa. Hiyo ndio principle ya ku-lay foundation ( kuweka msingi) na kushindwa kufanya hivyo kwa mujibu wa kesi ya Mohamed Shsrrif chain of custody inakatika.

Wakili Kaunda: Mahakama isije kuingia kwenye mtego wa kufanya kile ambacho imeombwa na prosecution

Wakili Kaunda: Mheshimiwa Jaji mwaka Jana mwezi wa Tisa Mahakama ya Tanzania iliandaa mwongozo wa maadili...

Wakili Hilla anapinga kuwa ni hoja mpya na hawatapa nafasi ya kuijibu na jaji anakubaliana na pingamizi hilo kuwa hawatapata nafasi na wakili Kaunda anaendelea.

Kwa mara nyingine Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando anasimama kupinga lakini kabla hajatoa hoka yake Jaji Tiganga anamwelekeza wakili Kaunda kuwa anatoka kwenye reli na wakili Kaunda anafunga hoja zake.

Wakili Kibatala: Nimesikiliza hoja za Wakili wa Serikali Hilla lakini kuna hoja moja hajaijibu. Kwamba DR hii ni document ambayo iko exhibit room hata kama iko hapa lakini imejikuta tu iko mikononi mwa afisa wa polisi.

Hatapinga kuwa kuna hatua walipaswa kuzitumia kutoa kifaa stoo ya mahakama bali amehamisha tu mzigo wa uthibitisho

Kwangu kuwa sijatoa kifungu lakini hata yeye hajatoa permissive rule.

Kwa hiyo Kuna hatua walipaswa kuzifanya kukitoa kifaa kile stoo kiwe kwanza kwenye custody ya mtu yeyote ndipo wakiombe.

Kwa hiyo hawajapinga hilo na linabaki bila kupingwa.

Hatukatai trial within trial ya Adamu maarufu Adamoo ni sehemu ya main case, lakini hata shahidi huyu hajaeleza uhusiano wake na shahidi aliyeitoa document hiyo kwenye trial ya within trial ya Adamoo.

Baada ya trial within trial ya Adamoo exhibit hiyo maana yake iliwekwa stoo kwa hiyo tunasisitiza haijamfikia shahidi sasa sawa..

Wakili Kibatala:  Kuhusu hoja kwamba sijaonesha prejudice ya hatua hiyo ni kwamba Bunge lilitunga sheria na Kanuni za uendeshaji Mashauri na zinapokiukwa hiyo ndio prejudice yenyewe na washtakiwa wana haki ya kukimbilia kwenye mfumo wa sheria unaotabirika

Jaji Tiganga: Nimesikiliza hoja zenu, na naomba nipate muda wa kuzipitia na kuandika uamuzi.

Kwa hiyo nitaahirisha shauri hili hadi kesho asubuhi kwa ajili ya kutoa uamuzi na ningeomba muda uwe saa 5 asubuhi.