Mawaziri wang’ara NEC-CCM

Wageni waalikwa wakiwa ndani ya ukumbi wa Jakaya Kikwete walipohudhuria Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Wakati CCM ikifanya uchaguzi wake wa ndani jijini Dodoma, idadi kubwa ya nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) zimechukuliwa na mawaziri.

Dar es Salaam. Wakati CCM ikifanya uchaguzi wake wa ndani jijini hapa, idadi kubwa ya nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) zimechukuliwa na mawaziri.

Uchaguzi huo umefanyika katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Jijini Dodoma ambapo nafasi za ujumbe, makamu mwenyekiti na mwenyekiti wa chama hicho zilikuwa zikigombewa.

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Dk Ali Mohamed Shein amewataja walioshinda kuwa ni  Angelah Kairuki ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Ashatu Kijaji (Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezekezaji), Angelina Mabula (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).

Wengine ni pamoja na Waziri wa Nishati, January Makamba, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Innocent Bashungwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Hata hivyo, baadhi yao wameanguka akiwamo Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene na Waziri wa zamani, William Lukuvi.