Mazao yaingiza Sh6.4 bilioni Manyara

Muktasari:

  • Mazao ya biashara yaliyotokana na vyama vya ushirika mkoani Manyara, kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 yameingiza kiasi cha Sh6.4 bilioni.


Babati. Mazao ya biashara yaliyotokana na vyama vya ushirika mkoani Manyara, kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 yameingiza kiasi cha Sh6.4 bilioni.

Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara, Venance Msafiri ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 25, 2022 mjini Babati kwenye jukwaa la maendeleo ya ushirika lililofanyika kwa siku mbili.

Msafiri amesema fedha hizo zimepelekwa kwa wakulima wa mazao hayo huku halmashauri za mkoa huo zikipata Sh194.8 milioni kutoka kwenye chanzo cha ushuru.

Ameyataja mazao yaliyofanya vizuri sokoni ni ufuta, alizeti, ngano, miwa, pamba, shayiri na kahawa.

Amesema kwa msimu wa mwaka 2021/2022 mazao yaliyouzwa kwenye vyama vya ushirika, ni tani 75,000 za miwa na kupatikana Sh3.9 bilioni na tani 46,000 za kahawa Sh391 milioni.

“Ngano ilipatikana tani 300 za Sh270 milioni, pamba tani 231,860 sawa na Sh278.2 milioni, alizeti tani 300 za Sh300 milioni, shairi tani 1,244 za Sh240 milioni na ufuta tani 84,000 za Sh248 milioni,” amesema Msafiri.

Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange amesema vyama vya ushirika vinafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wakulima