Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazingira wezeshi yatajwa kusaidia wawekezaji sekta ya madini

Mwekezaji wa madini wilayani Longido mkoani Arusha, Sendeu Laizer akizungumza na wananchi katila Kijiji cha Mundarara wilayani humo juzi.

Muktasari:

  • Baadhi ya viongozi wa mila wa kabila la Wamasai wilayani Longido mkoani Arusha wamepongeza uwekezaji wa uchimbaji wa madini wilayani humo uliowezesha kupatikana kwa ajira kwa wakazi wa kijiji cha Mundarara.

Longido. Baadhi ya viongozi wa dini na mila wilayani Longido Mkoa wa Arusha wamefanya dua maalum, wakiishukuru Serikali kwa kuwekewa mazingira rafiki yanayowawezesha wachimbaji madini kwa faida.

Akizungumza katika dua hiyo iliyofanyika Novemba 24, kiongozi wa mila la kabila la Wamaasai wilayani humo (Laigwanan), Peter Sengeyon amesema katika kijiji hicho cha Mundarara, familia zaidi ya 100 kutoka kijijini hapo zimenufaika na ajira katika mgodi wa mwekezaji Bilionea Sendeu Laizer.

"Tunashukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wachimbaji kwani sisi wa Mundarara na Longido kwa ujumla, tumeshuhudia vijana zaidi ya 100 wakijishughulisha na shughuli za uchimbaji kule mgodini kwa Laizer, hivyo familia zao zinanufaika kupitia yeye.

"Mungu ametubariki leo kupitia yeye makundi mengi ya kijamii ikiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuchangia mradi wa maji na shule, tunaomba na wafanyabishara wengine wachangie katika shughuli za kijamii, hii tumeweza kufanya kutokana na amani ambayo tuko nayo katika nchi yetu," amesema Sengeyon.

Kwa upande wake Bilionea Laizer amesema mazingira rafiki na amani iliyopo nchini inawezesha wachimbaji kufanya shughuli zao kwa uhuru na wananchi wamekuwa wakinufaishwa na miradi ukiwemo ya ujenzi wa shule, maji na elimu kwa watoto wanaotoka katika familia duni na yatima inayotekelezwa na mwekezaji huyo.

"Sisi wawekezaji katika wilaya hii na nchini kwa ujumla tunafanya shughuli zetu bila kuwa na usumbufu wa aina yoyote kutokana na mazingira haya rafiki tuliyowekewa na Serikali kuvutia wawekezaji," amesema Laizer.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Longido, Papa Nakuta amesema Serikali imepeleka miradiya maendeleo ya zaidi ya Sh14 bilioni kwa ajili ya mkoani Arusha, huku akimpongeza mwekezaji huyo kwa uhusiano mzuri baina yake na jamii inayomzunguka.