Mbowe akwaa kisiki Mahakama ya ufisadi

Mbowe akwaa kisiki Mahakama ya ufisadi

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, kwa ajili ya kusikiliza uamuzi dhidi ya pingamizi waliwasilisha mahakamani hapo la kupinga kesi yao kusikilizwa na mahakama hiyo .

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu ‘mahakama ya mafisadi’, imetupilia mbali pingamizi ililowasilisha na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu la kutaka kesi inayowakabili isikilizwe na mahakama hiyo kwakuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi zenye mashtaka ya ugaidi.

Uamuzi huo umetolewa leo, Septemba Mosi, 2021 na Jaji Elinaza Luvanda ambaye baada ya kupitia hoja za pande zote mbili amesema Mahakama yake ina mamlaka ya kusikiliza Mashauri ya ugaidi na kwamba pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi halina mashiko na hakubaliani nalo.