Mbowe: Bila tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya hatushiriki uchaguzi wowote

Thursday May 27 2021
MBOWEPIC

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akizungumza na wajumbe wa chama hicho kwenye mkutano uliofanyika mkoani Arusha jana. Na Mpigapicha wetu

By Zourha Malisa

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama hicho hakitashiriki uchaguzi wowote kama hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya.

Akizungumza na  viongozi wa kamati ya utendaji ya mikoa ya Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Arusha juzi, Mbowe amesema “ndugu zangu tunahitaji kufanya movement ya Katiba na tume huru ya uchaguzi, tumesema hatutakwenda kwenye uchaguzi wowote na tume hii.”

“Tutafundisha makada wetu kuanzia ngazi ya chini umuhimu wa Katiba na ulazima wa Katiba. Katiba yetu inaruhusu Rais wa kifalme ambaye ana madaraka makubwa kuliko Katiba.

Nimemwambia mama Samia Suluhu Hassan, mama mambo ya Katiba si mapenzi yako ni mapenzi ya Taifa, tutaitafuta, tutaipigania Katiba ya nchi yetu kabla ya uchaguzi wa 2025. Tunajipanga.” amesema Freeman Mbowe


Advertisement