Mbunge agawa majiko 110 ya gesi Chunya

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi aliyevaa Epron ya mamantilie pembeni akiwa na muwakilishi wa kampuni ya oryx gesi wakimkadhi zawadi ya jiko la gesi katibu tawala Wilaya ya Chunya Anacreti Michombero. Picha na Mary Mwaisenye Chunya

Muktasari:

  • Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi ametoa majiko ya gesi chapa Oryx 110 kwa mama lishe wilayani Chunya Mkoa Mbeya pamoja na kuwapatia kilo tano za mchele na fedha Sh30, 000 kwa washindi watano ikiwa ni kampeni ya ‘Maryprisca Mamantilie festival’.

Chunya. Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi ametoa majiko ya gesi chapa Oryx 110 kwa mama lishe wilayani Chunya Mkoa Mbeya pamoja nakuwapatia kilo tano za mchele na fedha Sh30, 000 kwa washindi watano ikiwa ni kampeni ya ‘Maryprisca Mamantilie festival’.

Hata hivyo, Maryprisca ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mbeya amesema kampeni hiyo haina malengo ya kisiasa bali kuwainua wanawake kiuchumi.

Mahundi ameyasema hayo leo Oktoba 10 2023 wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika katika mamlaka ya mji mdogo Makongolosi lililowakutanisha mamalishe kutoka kata zote wilayani humo.

Amefafanua kuwa kampeni hiyo ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT), Mary Chatanda aliyewataka wabunge wa viti maalumu watoke kumsaidia Rais kufanya kazi.

“Nafahamu mtumiaji mkuu wa kuni na mkaa ni mwanamke hasa katika shughuli za mamantilie hivyo nimeona nije na njia mbadala ya kuwapatia jiko la gesi bure ili liweze kuwasaidia katia shughuli zenu.

“Ikiwa ulikuwa unatumia mkaa wa Sh45,000 kwa kwa ununuzi ya mkaa kwa  mwezi jiko la gesi utatumia Sh25,000 hivyo itakusaidia kuweka akiba na kukuza biashara zao,amesema  Naibu Waziri wa Maji Mahundi," amesema.

Wakizungumza na Mwananchi katika kampeni hiyo, baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye kogangamano hilo la kuwakutanisha mamalishe wamempongeza mbunge huyo.

“Tunampongeza Mbunge kwa kutuletea majiko na kwa mchele aliotupatia, kwani ametuongezea mitaji katika biashara yetu,” amesema Grace Swila ambaye ni mama lishe wa eneo hilo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Mamlaka ya mji Mdogo wa Makongolosi, Linus Mwanitega amempongeza Naibu Waziri Mahundi kwa namna anavyojitoa kuwawezesha wanawake wa wilaya hiyo.

"Nakufahamu vizuri tangu ukiwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya umekuwa mtu wa watu siku zote naona hujabadikika, Mungu azidi kukutumia kuwafikia wananchi wa chini,” amesema Mwanitega.