Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge atwishwa zigo bei ya kahawa kuporomoka sokoni

New Content Item (1)
Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kigina Kata Ntobeye mpakani mwa Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi. Picha na Anania Kajuni.

Muktasari:

Wakulima wa kahawa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamemtwisha mbunge wao zigo la kuwasaidia kutatua tatizo la kuporomoka kwa bei ya kahawa kutoka Sh3, 020 ya awali hadi Sh1, 900.

Ngara. Wakulima wa kahawa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamemtwisha mbunge wao zigo la kuwasaidia kutatua tatizo la kuporomoka kwa bei ya kahawa kutoka Sh3, 020 ya awali hadi Sh1, 900.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kigina Julai 22, 2023 na kuhutubiwa na Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro, baadhi ya wakulima wamedai kuporomoka kwa bei ya kahawa kunawapa hofu ya kupata hasara kutokana na gharama kubwa ya uzalishaji kulinganisha na bei iliyoko sokoni.

“Wakati bei ya kahawa aina ya Arabica imeshuka sokoni kutoka Sh3, 020 ya awali hadi Sh1, 900, gharama zingine za maisha ikiwemo mahitaji ya familia na pembejeo za kilimo zinazidi kupanda. Serikali lazima itafute namna ya kutusaidia wakulima," amesema Ramadhan Abdul mkulima wa kahawa kutoka kijiji cha Kigina 

Amesema wakulima wanatambua jitihada za kutafuta soko na bei nzuri zinazofanywa na chama cha ushirika cha Ngara Farmers cooperative Society, ni vema Serikali na wadau wengine kusaidia kutatua tatizo hilo kwa faida na maslahi ya wakulima na Taifa kwa ujumla.

Mkulima mwingine, Justus Rwechungura amepongeza jitihada za Serikali za kusambaza pembejeo za kilimo kwa wakulima, lakini akashauri juhudi hizo zihusishe utafutaji na uhakika wa soko la mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi.

"Hakutakuwa na faida kwa Taifa kuongeza uzalishaji sekta ya kilimo bila uwepo wa soko la uhakika na lenye bei nzuri," amesema Justus 

Akizungumzia kupomoka kwa bei ya kahawa, Mbunge Ruhoro amewashauri wakulima kuuza mazao yao kwa bei iliyopo ili kuepuka hasara zaidi iwapo bei itaendelea kushuka kwenye soko la dunia.

"Soko la kahawa yetu inategemea pia soko la dunia ambalo hivi sasa limekumbwa na mtikisiko wa kiuchumi kutokana na sababu kadhaa ikiwemo vita vya Urusi na Ukraine," amefafanua Ruhoro

Amesema kutokana na ukweli huo, kuna hatari ya bei ya bidhaa ikiwemo za kilimo kuendelea kuporomoka katika soko la dunia; hivyo kuwashauri wakulima kuuza kahawa yao kabla bei haijashuka zaidi.