Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge Babati ataka uchunguzi wa mapato ya minara Sigino

Mbunge wa Babati mjini mkoani Manyara, Emannuel Khambay akizungumza na wakazi wa kijiji cha Sigino juu ya changamoto ya minara ya simu redio na luninga kutolipia ushuru. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Minara ya redio, luninga na mitandao ya simu imewekwa katika kijiji cha Sigino mjini Babati mkoani Manyara ila malipo yao hayaonekani.

Babati. Mbunge wa Babati mjini mkoani Manyara, Emmanuel Khambay ameagiza ofisi ya mkurugenzi wa mji huo kufanya uchunguzi juu ya mapato ya fedha za minara ya simu, redio na luninga.

Khambay ameagiza hayo alipofanya ziara katika Kata ya Sigino leo Julai 26, 2026 ili kuzungumza na wananchi wa eneo hilo, kusikiliza na kutatua kero na changamoto zao mbalimbali.

Ameeleza kuwa siyo vyema minara ya redio, luninga na mitandao ya simu iliyowekwa kwenye kijiji cha Sigino ila malipo ya ushuru unaolipiwa hayaonekani hivyo ofisi ya mkurugenzi ifuatilie hayo.

 Amesema uchunguzi wa kina unapaswa kufanywa ili kubaini namna ambavyo kijiji kinaweza kunufaika na minara yote iliyopo eneo hilo na fedha zake zionekane.

"Hii minara ni chanzo cha mapato kwenye kijiji kwani ni uwekezaji unafanyika hivyo fedha hizo zingepunguza adha ya wanakijiji kuchangia fedha za maendeleo," amesema Khambay.

Akizungumza kwenye ziara hiyo mkazi wa Sigino, Juma Aron, ameeleza kuwa mapato ya minara yapo lukuki kwenye kijiji hicho ila wanapatiwa mapato ya mnara mmoja pekee.

"Tunashukuru kwa hatua hiyo mbunge wetu kwani kijiji chetu kimekuwa na milima ambayo ina minara mingi ila mapato kulipwa imekuwa changamoto," amesema Aron.

Mkazi mwingine, Mariam Seleman amepongeza agizo la mbunge huyo kwani wanaamini uchunguzi utafanyika na hatua kuchukuliwa.

"Minara ya simu ya mitandao mbalimbali redio kubwa nchini na vituo vya luninga wametegesha minara yao kijiji kwetu, ila mapato yake hatujayaona," amesema.

Pia, mbunge huyo amekabidhi fulana na bukta za michezo kwa vijana wa kijiji hicho cha Sigino ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono michezo na vipaji.