Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge CCM ataka muda wa kuthibitisha wagonjwa wa akili kupunguza

Mbunge CCM ataka muda wa kudhibitisha wagonjwa wa akili kupunguza

Muktasari:

Mbunge wa viti maalumu CCM, Lucy Mayenga ameitaka Serikali kupunguza muda wa kuthibitisha wagonjwa wa akili walioko kwenye magereza mbalimbali nchini.

Dodoma. Mbunge wa viti maalumu CCM, Lucy Mayenga ameitaka Serikali kupunguza muda wa kuthibitisha wagonjwa wa akili walioko kwenye magereza mbalimbali nchini.

Mayenga ameyasema hayo leo Jumatano Februari 3, 2021 wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni mjini Dodoma katika kikao cha pili cha Bunge la 12.

Amesema kuna wafungwa wanaougua ugonjwa wa akili  na wapo katika kundi la kisheria lakini udhibitisho umekuwa ukichukua muda mrefu huku akihoji mkakati wa Serikali kupunguza muda wa kuwahudumia wagonjwa hao.

Akijibu swali hilo Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima amesema wamelichukua na watalifanyia kazi ili watu hao waweze kupata huduma mapema.

Katika swali la msingi, mbunge wa viti maalum CCM,  Mariam Kisangi  amesema Tanzania imekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa afya ya akili, “nini chanzo cha ugonjwa huo, je  Serikali ina utaratibu gani wa kuwasaidia wagonjwa wa afya ya akili.”

Akijibu swali hilo naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema kitaalamu  hakuna  sababu  moja  inayoweza  kusababisha ugonjwa wa afya ya akili.

Amesema sababu za kibailojia,  uwepo  wa  vinasaba katika mwili  vinaongeza  uwezekano wa mtu kupata ugonjwa  wa  afya  ya  akili.

Nyingine ni  maradhi  ya  muda  mrefu  na  matumizi  ya  vilevi  kama  bangi, pombe  na  aina  nyingine  za  vilevi  zinaweza  kuwa  vichocheo  hasa  kwa  mtu  mwenye vinasaba vya uhatarishi wa ugonjwa.

Dk Mollel amesema Serikali iliandaa sheria  inayosimamia  utoaji  wa  huduma  za  afya  ya  akili  mwaka  2008 inayotoa mwongozo  na  utaratibu  wa  namna  ya  kuwapokea  na kuwahudumia watu wenye ugonjwa wa akili.

Pia Serikali imehakikisha kuwa huduma za matibabu ya ugonjwa wa afya ya akili ikiwa ni  pamoja  na  dawa  zinatolewa  kuanzia  ngazi  ya  hospitali  za  rufaa  za  mikoa  hadi hospitali maalum ya Taifa ya afya ya akili Mirembe.

Amesema pia Serikali itaendelea kutoa elimu kuhusu ushiriki wa wazazi katika kuwalea watoto na kuongeza  udahili  wa  wanafunzi  wa  uzamivu  kutoka  wanafunzi  watatu hadi watano ilipofika mwaka 2015 na kufikia udahili wa wanafunzi 10  hadi 15 kwa mwaka ilipofika  2020.

Amesema pia Serikali imeongeza  idadi  ya  vyuo  vikuu  vinavyotoa  shahada  ya  uzamivu kutoka kimoja mwaka 2015 hadi kufikia vyuo vitatu mwaka 2020.