Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge Toufiq akomalia ujenzi kiwanda cha mafuta

Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Toufiq akizungumza leo bungeni Ijumaa Septemba1, 2023.

Muktasari:

  • Ni mara kadhaa mbunge huyo amekuwa akililia ujenzi na upanuzi wa Viwanda vya mafuta ya alozeti ili kutoa tija kwa wakukima.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Toufiq amehoji Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha mafuta ya kula yanazalishwa nchini kwa wingi.

Leo Ijumaa Septemba Mosi, 2023 mbunge huyo amehoji namna gani Serikali itawasaidia wakulima wa mazao yanayozalisha mafuta ya kula ili waongeze uzalishaji zaidi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutekeleza mkakati wa kuendeleza sekta ndogo ya Alizeti na Chikichi ambayo ndiyo mazao makubwa yanayoweza kuzalisha kwa tija mafuta ya kula hapa nchini.

Naibu Waziri amesema katika utekelezaji wa mkakati huo, viwanda vipya, kama

Qstec na Jeolong vimeanzishwa ikiwemo upanuzi wa viwanda kama Mount Meru Millers.

Amesema Serikali imeongeza nguvu katika Taasisi za utafiti wa mbegu na hivyo kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za alizeti na michikichi.

Kigahe amesema kwa sasa serikali imeelekeza nguvu zaidi kwenye kilimo cha kuzalisha mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya malighafi katika viwanda vya ndani.