Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchungaji akamatwa tuhuma za kulawiti mtoto

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga (RPC), Janeth Magomi

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikiria Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Makedonia ya Lubaga, Mjini Shinyanga, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka nane.

Shinyanga. Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikiria Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheri Tanzania (KKKT), Makedonia ya Lubaga, Mjini Shinyanga, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka nane.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga (RPC), Janeth Magomi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa  jana Ijumaa Augosti 12, 2022 baada ya jeshi la Polisi mkoani humo kupokea malalamiko kutoka kwa moja ya familia za waumini wa kanisa hilo.

RPC Magomi amesema jeshi hilo linamshirikia mchungaji huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


"Jina tumelihifadhi kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi na tutakapokamilisha atafikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo," amesema Magomi.