Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani

Muktasari:

  • Membeamesema yuko njiani kurudi mahali fulani ambapo hakupataja, huku akisema anasubiri uamuzi wa shauri lake lililoko mahakamani hapo Oktoba 12 mwaka huu.

Lindi. Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ACT Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa 2020, Benard Membeamesema yuko njiani kurudi mahali fulani ambapo hakupataja, huku akisema anasubiri uamuzi wa shauri lake lililoko mahakamani hapo Oktoba 12 mwaka huu.

Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika utawala wa awamu ya nne, ameyasema hayo leo Oktoba 5 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rondo Mkoani Lindi, baada ya kukaribishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye yuko ziarani mkoani humo.

"Niwaombe tusahau yaliyopita kuanze upya tujenge rondo na taifa letu Niko tayari kuwa kampeni meneja wake rais uchaguzi mkuu mwaka 2025," alisema Membe.

Membe alihamia ACT Wazalendo Julai 15, 2020 baada ya kurudisha kadi ya CCM Julai 6, akiwa ameshafukuzwa CCM Februari 2020, huku baadhi ya waliokuwa makatibu wakuu wa chama hicho, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana wakipewa karipio na chama hicho.

Hata hivyo, safari yake ndani ya ACT Wazalendo iliingia dosari, alipositisha kampeni zake katika hatua za awali, jambo lililowakasirisha viongozi wa chama hicho, huku mwenyewe akijitetea kuwa atafunga bao katika dakika za mwisho.

Safari ya Membe ndani ya ACT Wazalendo ilikamilika Januari 2021 alipotangaza kujitoa kwenye chama hicho.

Akizungumza katika mkutano huo, Membe amemfananisha Rais Samia kama mhandisi wa umeme aliyewasha swichi iliyokuwa imefungwa na kuifanya Membe alisema sasa Tanzania imeanza kuonekana kwenye uso wa kimataifa, kidemokrasi mahusiano ushirikiano wa kimataifa.

Ameendelea kusema kuwa wakati wote yuko tayari yeye na wananchi wa Rondo kumpa ushirikiano Rais na serikali yake kwa kuwa ameonyesha dhamira ya kuirudisha nchi kwenye misingi ya umoja, mshikamano na mahusiano ya kitaifa na kimataifa.

Amemuomba Waziri Mkuu Majaliwa kufikisha salamu na pongezi kwa Rais samia suluhu kwa kazi mzuri anayofanya

Kwa upande wake Waziri Wkuu Majaliwa alisema amezipokea pongezi hizo kwa niaba ya rais na hatazifikisha kwa raisi na kuwaomba wananchi wa Rondo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya, elimu, mbiundombinu.

"Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya na miundombinu," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.