Mfanyabiashara Mohamed Raza afariki dunia

Marehemu Mohamed Raza enzi za uhai wake

Muktasari:

  • Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mwanasiasa aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Raza amefariki dunia leo Juni 8, 2023 Saa tano asubuhi katika Hospital ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mwanasiasa aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mkoa wa Kusini Unguja, Mohamed Raza amefariki dunia leo Juni 8, 2023 Saa tano asubuhi katika Hospital ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za msiba huo ambazo zimethibitishwa na mmoja wa wanafamilia aliyejitambulisha kwa jina la Mohammed Ibrahim Raza, maziko yake yanafanyika Saa 11 jioni katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.

“Ni kweli ndugu yetu aametutoka tunategemea kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kisutu leo saa 11 jioni,” amesema Mohamed

Mei 9, 2023, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alifika katika Hospitali ya Aga Khan alikokuwa amelazwa kwa lengo la kumjulia hali.

Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.