Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfumo wa IDRAS kuunganishwa na AI, kulinda taarifa binafsi

Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Maro akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya matumizi ya Mfumo Jumuishi wa usimamizi wa mapato ya ndani (IDRAS).

Muktasari:

  • Mfumo Jumuishi wa usimamizi wa kodi za ndani (IDRAS) wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) umeunganishwa na akili unde kumsaidia mlipakodi kupata majibu ya maswali kuhusu kodi bila kwenda ofisini.

Shinyanga. Katika kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi kwa wafanyabiashara kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeunganisha mfumo wa IDRAS pamoja na akili unde ili kumsaidia mlipakodi kupata majibu ya maswali kwa urahisi bila kwenda ofisini pamoja na kulinda taarifa zake.

Akizungumza leo Januari 27, 2026 katika mafunzo ya matumizi ya Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) kwa wafanyabiashara na walipakodi, mwenyekiti wa mafunzo ambaye ni Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro ameeleza kuwa hii inaongeza uwazi na uelewa kwa mlipaji na kumfanya kulipa kodi kwa hiari.

Pichani ni walipa kodi wakiwa katika mafunzo ya ya matumizi ya Mfumo Jumuishi wa usimamizi wa kodi za ndani, yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Picha na Hellen Mdinda.

“Mfumo wetu umeunganishwa na Akili unde (AI) ambapo itasaidia moja kwa moja mlipakodi kuuliza na kupata majibu ya maswali yanayohusiana na kulipa kodi, pia, hii inamfanya kuwa huru na salama katika kutunza taarifa za mlipakodi,” amesema Maro.

Kwa upande wake, mwezeshaji kutoka TRA, Omary Mataw ameeleza namna ya kujisajili katika mfumo huo akisema mzazi ana uwezo wa kupata namba ya mlipakodi (TIN Number) ya mtoto, ambayo itaenda kwa mtoto akifikisha miaka 18, na kukamilisha usajili wa maelekezo mengine, pia, kwa wenye TIN watatakiwa kuweka upya nywila.

Mfumo wa IDRAS unatarajiwa kuanza Februari 9, 2026 ikiwa ni hatua ya kuboresha ulipaji kodi kuendana na maendeleo ya kidijitali, ukiwa na lengo la kurahisisha utoaji wa huduma, kuongeza uwazi na uelewa kwa walipakodi kulipa kwa hiari, ambapo huduma kupitia mfumo utakuwa unafanyika kielektroniki kwa saa 24.