Mgongolwa: Upelelezi bado ni wimbo uliozoeleka kortini

Muktasari:
Mbali na Kitilya aliyewahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka manane likiwamo la utakatishaji wa Dola 6 milioni za Marekani ni Shose Sinare na Sioi Solomon.
Dar es Salaam. Wakili wa kujitegemea, Alex Mgongolwa ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi inayomkabili Harry Kitilya na wenzake wawili kuwa upelelezi kutokamilika ni wimbo uliozoeleka mahakamani hapo ambao hutolewa kila siku na mawakili wa Serikali.
Mbali na Kitilya aliyewahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka manane likiwamo la utakatishaji wa Dola 6 milioni za Marekani ni Shose Sinare na Sioi Solomon.
Wakili Mgongolwa alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya Wakili wa Serikali, Elia Athanas kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.