Miaka 70 ya Malkia Elizabeth katika uongozi

Muktasari:

  •  Licha ya kufariki akiwa na umri wa miaka 96, Malkia Elizabeth II wa Uingereza ndiye mkuu wa nchi anayeshikilia rekodi ya dunia kuhudumu muda mrefu zaidi maradakani.


Dar es Salaam. Licha ya kufariki akiwa na umri wa miaka 96, Malkia Elizabeth II wa Uingereza ndiye mkuu wa nchi anayeshikilia rekodi ya dunia kuhudumu muda mrefu zaidi maradakani.

Elizabeth II aliukwaa wadhifa wa malkia akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 1952 baada ya kifo cha baba yake, aliyekuwa mfalme wa taifa hilo George VI.

Hadi anafariki katika visiwa vya Balmoral nchini Scotland alikokuwa anapatiwa matibabu, Elizabeth II ameiongoza Uingereza kwa miongo saba.

Mwaka 2015, alikuwa kiongozi wa kwanza wa Uingereza aliyehudumu muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo, akivunja rekodi iliyowekwa na babu wa babu yake Malkia Victoria na ndiye aliyekuwa mkuu wa nchi mzee zaidi duniani.

Pia amevunja rekodi ya Malkia Victoria, bibi wa babu yake, aliyetawala kwa miaka 63

Mwanaye wa kwanza Charles aliyekuwa mfalme wa Wales ndio atakuwa mfalme wa taifa hilo, kulingana na tamaduni za nchi hiyo.

Elizabeth II alizaliwa April 21, 1926 jijini London nchini humo.

Mbali na majukumu yake ya kiutawala, Elizabeth II alikuwa mke na mama wa watoto wanne, kadhalika bibi wa wajukuu nane na vitukuu 12.

Juhudi za utendaji wake wa kuufanya utawala wa kifalme ubaki kuheshimika licha ya mabadiliko ya kijamii, teknolojia na uchumi, ni moja miongoni mwa mambo yatakayobaki alama ya maisha yake ya utumishi.