Miamala ya fedha yapanda, Bunge laelezwa

Muktasari:

  • Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu leo Jumanne, Januari 31, 2023, imewasilisha taarifa yake yam waka 2022 bungeni jijini Dodoma na kueleza juu ya mambo mbalimbali ikiwemo mwenendo wa miamala ya fedha.

Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imesema idadi ya miamala ya fedha ilipanda kutoka Sh349.9 milioni Julai, 2022 hadi kufikia miamala Sh410.74 bilioni kwa Desemba, 2022. 
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa kamati hiyo Miraji Mtaturu akisoma taarifa ya mwaka ya kamati ya Bunge ya Miundombinu leo Jumanne Januari 31, 2023, bungeni jijini Dodoma.
Amesema pia idadi ya watumiaji wa miamala ya simu iliongezeka kutoka milioni 38.40 Julai hadi milioni 40.95 Desemba 2022.
Aidha, Mtaturu ametaka kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya Reli kuruhusu sekta binafsi kuwekeza katika kutoa huduma za reli.
Pia, ametaka Serikali kuongeza bajeti ili kukabiliana na ufinyu wa bajeti kwa taasisi zilizo katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kunakosababisha kukwamisha utekelezaji wa majukumu na miradi mbalimbali.
Ametoa mfano wa miradi hiyo ni ile inayotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Mfuko wa Barabara Tanzania (Roadfund).