Miguna Miguna arudi Kenya

Muktasari:

  • Mwanasheria huyo machachari amefanikiwa kurejea nchini Kenya baada ya kupita zaidi ya miaka minne akiwa kizuizini nchini Canada tangu mwaka 2018.

Nairobi. Mwanasheria na mwanaharakati wa Kenya, Dk Miguna Miguna amerejea nchini humo.

 Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) leo Oktoba 20, Miguna aliyekuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka minne nchini Canada baada ya kufukuzwa tangu mwaka 2018, ameshukuru Rais wa nchi hiyo, William Ruto kwa kumruhusu kuingia nchini humo.

Mwanasheria huyo machachari amesema ilichomtokea hakitakiwi kumtokea mtu mwingine yeyote.

Miguna alifukuzwa nchini Kenya mwaka 2018 baada ya kushiriki katika mkutano haramu wa kumwapisha Raila Odinga kuwa ‘Rais wa watu’ katika bustani ya Uhuru Park baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Alishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na uhaini na majaribio yake ya kurejea nchini humo licha ya maagizo kadhaa ya mahakama yaliyotolewa kuidhinisha kurejea kwake ambako hakukufanikiwa.