Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikoa minne yapokea miti milioni moja kulinda mazingira

Muktasari:

Wakulima laki moja wanufaika na upandaji miti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kujiinua kiuchumi.

Kilolo. Jumla ya wakulima laki moja kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe wamenufaika na mpango wa upandaji miti ya matunda, mbao na miti ya kurutubisha udongo kwa lengo la kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kuinua kipato cha wakulima.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya One Acre Tanzania Limited, Dorcas Tinga wakati wa usambazaji wa miche hiyo akisema miti itakavyopandwa kwa wingi zaidi ndivyo itasaidia kupunguza au kuepukana na changamoto ya zinazotokana na madadiliko ya hali ya tabia nchi nchini.

Amesema kwa msimu huu pekee wamesambaza miche milion moja kwa mikoa minne ambayo ni Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe ambapo Wilaya ya Kilolo imesambaziwa miche 500,000.

“Sasa hivi kama tunavyoshuhudia dunia nzima inapitia katika changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi tunaamini wakulima kwa kupanda miti zaidi watajiweka katika nafasi nzuri ya kuhakikisha licha ya mabadiliko haya wao wanakuwa na nafasi ya kupata tija kupitia kilimo cha miti.”

“Miti mingine ni ya mbao ambapo wamelenga wakulima kupata mapato zaidi kwa maana ya kwamba mkulima asitegemee mahindi na  maharage lakini pia anakuwa na mazao ya kibiashara ambayo ataweza kunufaika nayo kwa miaka mingi zaidi,”

Tinga amesema kuwa msimu huu wanatoa miche ya aina tatu kwa wakulima ambayo ni miche ya matunda, mbao na miche kwa ajili ya kurutubisha ardhi.

“Hii miche yote mitatu tunaamini itakuwa na faida kwa wakulima kwa sababu kwanza parachichi ni zao la kimkakatati katika nchi yetu. Kwa hiyo sisi tunawawezesha wakulima kupanda parachichi zaidi kwa sababu itawasaidia wao kupata masoko kupitia serikali,” amesema.

Wakizungumza na wakati kupokea miti hiyo baadhi ya wakulima wamesema miti hiyo itawasaidia kuinua kipato cha familia zao miaka ya mbeleni.

Mkulima kutoka Wilaya ya Kilolo, Bruno Augustino amesema ameamua kupanda miti ya parachichi ambapo anatarajia kuvuna ndani ya miaka mitatu na kumpatia faida na kuinua kipato chake.

“Tunapanda miti hii ya mbao na inakua zaidi ya miaka 9. Hii ni kwa faida ya familia zetu kama sitokuwepo, watakaofaidika ni familia yangu. Pia kupitia kilimo cha maparachichi nitaanza kuona faida yake baada ya miaka mitatu ambapo nitavuna na zao nila mda mfupi,” amesema.

Kampuni ya One Acre Tanzania imeanza kugawa miche ya miti milioni moja katika mikoa ya Iringa, Mbeya Songwe na Njombe ikiwemo miparachichi na miti ya mbao ambayo wakulima wanakopeshwa na kulipa taratibu na miti ya kurutubisha udongo ambayo inatolewa bure kwa wakulima hao