Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikoa zaidi ya 20 ijipange kwa hali hii kwa siku 10

Muktasari:

  • Kwa saa 24 zijazo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kutakuwa na vipindi vifupi vya upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa Pwani ya Bahari ya Hindi ikijumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani na visiwa vya Mafia,Unguja na Pemba.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetaja mikoa zaidi ya 20 ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba itakayokuwa na hali ya ukavu na baadhi kupata mvua nyepesi na upepo mkali kwa siku 10 kuanzia leo Jumatatu Julai 21, 2025.

Mikoa iliyotajwa kushuhudia hali ya ukavu kwa siku 10 (Julai 21-30) kwa Kanda ya Ziwa Victoria ni Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza na Mara.

“Kwa nyanda za juu kaskazini-mashariki, mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa,” imeeleza taarifa ya TMA kuhusu mwelekeo wa mvua kwa siku 10.

Mikoa ya Pwani ya kaskazini inayojumuisha Tanga, maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam na visiwa vya Unguja na Pemba kunatarajiwa vipindi vya mvua nyepesi na upepo mkali maeneo machache.

Pia maeneo mengine ni magharibi mwa Tanzania ambapo TMA imeeleza mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora hali ya ukavu inatarajiwa.

“Kanda ya kati, mikoa ya Dodoma na Singida hali ya ukavu inatarajiwa. Nyanda za juu Kusini magharibi yenye mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa nako hali ya ukavu inatarajiwa,”taarifa ya TMA imeeleza.

Nako upande wa Pwani ya kusini yenye mikoa ya Mtwara na Lindi matarajio ni hali ya ukavu na vipindi upepo mkali.

Pia kanda ya kusini yenye Mkoa wa Ruvuma na maeneo ya kusini mwa Morogoro hali ya ukavu inatarajiwa.