Miradi ya Sh26 bilioni kufikiwa na Mwenge Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa akizungumza na Waandishi wa habari juu ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani humo.
Muktasari:
Miradi 57 ya maendeleo yenye thamani ya Sh26.3 bilioni itakaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru katika halmashauri nane za mkoa wa Kagera.
Bukoba. Miradi 57 ya maendeleo yenye thamani ya Sh26.3 bilioni itakaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru katika halmashauri nane za mkoa wa Kagera.
Miradi hiyo ni ya barabara, maji, afya na kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ameyasema hayo leo Agosti 4, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.
"Jumla ya miradi yote itakayozinduliwa, kukaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru ni 57, utakimbizwa kilomita 1200.4 katika wilaya zote zilizopo Kagera" amesema Mwassa
Amesema, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokewa katika wilaya ya Muleba Agosti 8, 2023 na kukimbizwa wilaya za Mkoa wa Kagera na Utakabidhiwa katika Mkoa wa Kigoma Agosti 16, 2023.
Mwassa amesema maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia zote ikiwemo miradi mbalimbali itakayozinduliwa, kukaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge huo.