Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mjadala madai madini ya Tanzanite kutoroshwa

Mwenyekiti wa chama cha wanunuzi na wauzaji madini Tanzania (TAMIDA), Sammy Mollel akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha

Muktasari:

Wadau wa madini ya Tanzanite wameiomba serikali kutumia taasisi zake kudhibiti wanaopotosha kwamba madini hayo yanatoroshwa  licha  ya udhibiti  katika uchimbaji na uuzaji.

Arusha. Wadau wa madini ya Tanzanite wameiomba serikali kutumia taasisi zake kudhibiti wanaopotosha   kwamba madini hayo yanatoroshwa  licha  ya udhibiti  katika uchimbaji na uuzaji.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi na Wauzaji  Madini Tanzania (Tamida), Sammy Mollel amesema athari za kuendelea  kufumbia macho upotoshaji huo ni kubwa.

Amesema  wadau wa madini  wamesikitishwa na taarifa hizo na  amewataka  Watanzania kutoa ushirikiano kuwabaini  wanaoeneza taarifa hizo.

“Tangu kujengwa  kwa ukuta katika eneo la Mirerani  mwaka 2017 na kufungwa kwa mitambo ya kielektroniki ya ulinzi kumesaidia  kuondoa mianya ya utoroshaji wa madini na kwa hali inayoonekana hapa hakuna utoroshaji unaoweza kufanyika kutokana na udhibiti mkubwa uliopo, taasisi zote za serikali zipo, mifumo yote imekamilika na inafanya kazi, huo utoroshaji unaodaiwa unafanyika wapi na kwa njia gani?"

"Kama mtu ana uhakika na taarifa hizo ni vizuri akatoa  ushirikiano kwa kutoa ushahidi namna madini hayo yanatoroshwa  pamoja na  kuonyesha mianya  yote   ili wanaohusika waweze kuchukuliwa  hatua na sio kutoa  taarifa  za kupotosha ambazo kwa tafsiri nyingine zinadhalilisha kazi yote iliyofanyika na uwekezaji wote uliopo," amesisitiza.

Naye ofisa madini mkazi Mirerani,  Menard Msengi amesema serikali imeweka ulinzi wa kutosha na mazingira  mazuri kuanzia kwenye miradi hadi kufika sokoni  katika kuhakikisha sheria zote zinafuatwa na kwa ulinzi uliopo  suala la utoroshaji  haliwezi  kufanyika hata kidogo.

Naye  mwenyekiti  wa chama cha wanunuzi wadogo wadogo wa madini Tanzania (Chamata), Jeremia Kituyo amesema taarifa za kuwepo kwa utoroshaji wa madini zinasababisha  washindwe kufanya biashara kwani zinawaondolea uaminifu  kwa  wateja.

"Tunasikitika sana na matamko yanayotolewa yasiyo na ushahidi  kwamba madini  yanatoroshwa...,  ni za  kutuvunja moyo  na kuharibu sura  ya biashara ya madini nchini," amesema.

Mhandisi migodi kutoka kampuni ya Franone Mining, Benezet Karyuka amesema uwepo wa ukumewasaidiauta umewasaidia ulinzi.