Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mjema ahimiza lishe bora, aonya watoto kunyweshwa ulanzi Iringa

Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sophia Mjema

Muktasari:

  • Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewataka wakazi wa Mkoa wa Iringa kuwapa lishe bora watoto ili kupambana na udumavu.

Mufindi. Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sophia Mjema amewakumbusha wananchi wa Mkoa wa Iringa umuhimu kuzingatia lishe bora ili kupambana na tatizo la udumavu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya, Viashiria na Malaria (TDHS) wa mwaka 2022 inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaonyesha asilimia 30 ya watoto wanadumaa nchini.

Mkoa wa Iringa unaongoza kwa kuwa na udumavu kwa asilimia 56. 9, Njombe asilimia 50.4 na Rukwa ni asilimia 49.8.

Mjema amesema hayo leo Jumamosi Mei 27, 2023 katika kikao cha Shina namba tatu, Tawi la Wambi, Mtaa wa Boma, wilayani Mufindi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo Mkoani Iringa.

Kwa mujibu wa Mjema, wazazi wamekuwa wakienda kwenye majukumu ikiwa ni pamoja na kujitafutia riziki, jambo ambalo ni jema kwa uchumi wa familia na nchi kwa ujumla.

Hata hivyo, amehoji kitendo cha wazazi na walezi kuwapatia watoto pombe aina ya ulanzi kuwa hakikubaliki lakini pia kinasababusha watoto kukosa lishe inayotakiwa.

Hivyo amewasihi: “…mtoto anapaswa apewe lishe bora, kina mama hakikisheni watoto wanakula vizuri," amesistiza.

Jana Mei 26, 2023 wakati akizungumza na wazee wa mji wa Mafinga, viongozi wa dini na wafanyabiashara, Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo aliwasisitiza suala la lishe.

"Limeni miti, uzeni mbao na msiweke benki hela zote, lishe ni muhimu. Mkuu wa Mkoa (Halima Dendego) ameninong'oneza kuwa udumavu ni changamoto Iringa,”amesema Chongolo.

Mbali na lishe aliwakumbusha viongozi juu ya umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara na kuepuka tabia zinazochangia maambukizi ya Ukimwi.

Awali baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwananchi walisema zipo changamoto nyingi zinazosababisha tatizo la udumavu.

"Wazazi wakibanwa na kazi wanasahau watoto hii huenda ikawa sababu," amesema Anitha Mgeni, mkazi wa Mtaa wa Boma