Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkalimani akwamisha kesi Wachina wanaodaiwa kuwateka wenzao

Raia wa China, wanaodaiwa kuwateka wenzao wawili, wakitolewa katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo Jumatano Juni 17, 2026.

Muktasari:

  • Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani wakiwa ndani ya gari ya polisi, aina ya Toyota Land Cruiser saa nne asubuhi

Dar es Salaam. Raia wanne wa China, Deng Anqing, Fan Zhong Hua, Zhang Jianjun na Deng Qiang wanaotuhumiwa kuwateka wenzao wawili ili kujipatia Sh50 bilioni, wameshindwa kusomewa mashtaka katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya kukosekana kwa mkalimani.

Hanging na wenzake wamefikishwa Mahakamani hapo leo Jumatano Juni 17, 2026 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Herieth Mwailolo wa Mahakama.

Raia hao wamefikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 13626 ya mwaka 2026, lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosekana kwa mkalimani wa Mahakama huku washtakiwa hao wakiwa hawajui Kiswahili na Kingereza, hivyo kusababisha Mahakama hiyo kuahirisha ili kutoa nafasi kumuandaa mkalimani.

Hata hivyo, mkalimani atakayetafutwa atatakiwa kutafsiri Kingereza na Kiswahili kwenda lugha inayotumika na washtakiwa ambayo ni ya kichina.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mwailolo ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Alhamisi Juni 18, 2026 kwa ajili ya washtakiwa kusomewa mashtaka yao.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakiwa ndani ya gari ya polisi aina ya Toyota Land Cruiser, saa nne asubuhi chini ya ulinzi wa polisi wenye silaha waliyovaa kiraia.

Ilipotifika saa saba kasoro mchana, washtakiwa walitolewa mahabusu na kupelekwa mahakamani, kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Washtakiwa walivyopelekwa mahakamani, walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Dhamili Masinde akisaidiana na Judith kyamba.

Hata hivyo, walipoingia mahakamani upande wa utetezi ulidai raia hao hawajui Kiswahili wala Kingereza, kwa hiyo wao wana mkalimani.

Hakimu Mwailolo baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, alikubaliana na upande wa Jamhuri wa kuahirisha kesi hadi kesho Alhamisi Juni 18, 2026 kwa ajili ya Mahakama kumuandaa mkalimani.

Hakimu Mwailolo amesema Mahakama ndiyo yenye jukumu la kutafuta mkalimani na sio vinginevyo.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Hakimu Mwailolo aliahirisha kesi hadi kesho na washtakiwa wamerudishwa rumande.