Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkazi mwingine mkoani Tabora auawa kwa kupigwa risasi

Muktasari:

Siku zipatazo sita baada ya kuuawa mfanyabiashara wa Asali , Mohamed Mustafa katika Manispaa ya Tabora,mkazi mwingine ameuawa kwa kupigwa risasi wilayani Kaliua.

Tabora.  Siku zipatazo sita baada ya kuuawa mfanyabiashara wa Asali , Mohamed Mustafa katika Manispaa ya Tabora,mkazi mwingine ameuawa kwa kupigwa risasi wilayani Kaliua.

Mkazi huyo Edward Ernest Dodo, ameuawa kwa kupigwa risasi mgongoni na watu ambao bado hawajajulikana katika kata ya Ichemba wilayani Kaliua.

Diwani wa kata ya Makingi,James Nundo,ambaye mkazi huyo anaishi kwenye kata yake,amesema alikuwa mjasiriamali na alienda kata jirani ya Ichemba kwenda kupata kinywaji.

"Alienda kustarehe na kukuta watu wengine ambao walivamiwa na watu wenye mapanga usiku "Amesema

Diwani Nundo ameeleza kuwa watu wasiojulikana,walivamiwa sehemu hiyo ambayo watu walikuwa wakipata kinywaji,wakiwa na mapanga walianza kuwatisha wanywaji na kuwakata mapanga hatimaye kumuua mkazi wake.

Amesema inaelekea mkazi wake alikuwa anakimbia na ndipo alipopigwa risasi mgongoni na kufariki.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo Cha Afya Cha Ulyankulu na taratibu zingine zimeachiwa vyombo vya Dola kushughulikiwa mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,Richard Abwao,amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa itatolewa baadae.