Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke adaiwa kumuua mume kisa hataki kumuacha

Mwanamke Holo Jilia (katikati) akiwa na mwenzake Maela Athanas (kushoto) maarufu kama Rasi, wakazi wa kijiji cha cha Kilolero B Wilaya ya Malinyi Mkoa wa Morogoro wakiwa wamesimama mbele ya wanakijiji baada ya kukamatwa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya Charles Maghashi (55) mkulima. Picha na Lilian Lucas.

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi limedai kuwa mke wa marehemu alikula njama ya kumuua mume wake na ndiye aliyemtuma mtuhumiwa wa mauaji kutekeleza mauaji hayo akitaka talaka ili akaolewe na mwanaume mwingine.

Morogoro. Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Maela Athanas (33) maarufu kwa jina la Rasi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha cha Kilolero B Wilaya ya Malinyi, akidaiwa kumuua Charles Maghashi (55) kwa kutumwa na mke wa marehemu Holo Jilia (45) kwa ahadi ya kulipwa Sh900,000.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 6 mjini hapa, Kamnada wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 29 mwaka huu majira ya usiku, ambapo inadaiwa mtuhumiwa alishatanguliziwa Sh50, 000 kama malipo ya awali.

Mkama amesema wakati polisi wakiendelea na doria wilayani humo, walipata taarifa ya kuwepo kwa mauaji hayo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote wawili.

Ameeleza kuwa mtuhumiwa Maela Athanas alifika nyumbani kwa marehemu Maghashi na kumkuta akiwa amelala sebuleni kwake na kuanza kumkata na kitu chenye nja kali sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo.

Aidha amedai polisi baada ya kupata taarifa hiyo na kuwakamata watuhumiwa walifanya uchunguzi na kubaini kuwa mke wa marehemu ambaye ni Holo alikula njama ya kutaka kumuua mume wake Maghashi na ndiye aliyemtuma Maela kutekeleza mauaji hayo.

Inadaiwa watuhumiwa Holo na Maela walifanya uhalifu huo kwa madai kuwa mume wake huyo alikataa kumuacha ili aolewe na mwanaume mwingine.